Mwanafunzi Mwanza aomba kuchangiwa matibabu

Kijana Dickson Vedastus
Kijana Dickson Vedastus 

Kijana mmoja Dickson Vedastus Mkazi mmoja wa Kirumba Mkoani Mwanza amewaomba watanzania kumchangia shilingi milioni 25 ili akatibiwe maradhi ya kibofu cha mkojo yanayombumbua kwa miaka kumi na saba sasa.
Kijana huyo ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Kirumba amesema fedha hizo zitamsadia kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu ambayo yameshindikana hapa nchini.
Kijana huyo amewahi kupatiwa matibabu katika hospitali mbalimbali hapa nchini bila mafanikio na ndipo madaktari wakamshauri kwenda nchini india kwa matibabu zaidi kutokana na ukubwa wa tatizo la maradhi yanayomsumbua.
Kwa yeyote ambaye ameguswa na maradhi ya kibofu cha mkojo yanayomkabili Dickson anaweza kuwasiliana naye kwa simu nambari 0762 32 45 27/0683 58 00 04.

Picha na Amicus Butunga, TBC Mwanza.

No comments

Powered by Blogger.