SAJUKI KUZIKWA IJUMAA NA WAZIRI FENELLA ATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA YA MAREHEMU

 Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wakiwasili nyumbani kwa Marehemu SAJUKI Tabata Bima jijini Dar es Salaam leo.
Mke wa marehemu Wastara aliyefunikwa kanga ilikuwa ni vigumu kuamini kama mumewe kipenzi hatamuona tena alikuwa  akilia muda wote na kufarijiwa na ndugu wa karibu nyumbani kwao Tabata Bima jijini Dar. kushoto ni mama wa marehemu Bi. Zaitun

Msanii wa filamu Tea na  mdau wa filamu nchini Zamaradi wa Clouds Fm  na kipindi cha Take One cha Clouds Tv
Wasanii wakiomboleza kushoto ni Monalisa
Dokii akiingia msibani
Bibi wa Marehemu akiiingia nyumbani
Sebuleni wanandugu wakiwa wanaomboleza

Aha we acha tu, anaovyoonekana kusema Yusuph Mlela
Wasanii hawa ndio walikuwa kwenye filamu ya mwisho ya merehemu ambayo haikutoka inaitwa Mwanasheria
Wastara yani ilikuwa ni vigumu kuvumilia na kujikuta akilia muda wote kushoto ni mama wa marehemu aitwae Zaitun
Sehemu ya mbele ya nyumba ya marehemu
Viti na mahema vikiletwa kwa ajili ya waombolezaji

Wasanii wakiwa wamejitokeza katika msiba wa mwenzao.
 
Watu waliojitokeza msibani huku wengine wakiwa wamekaa kwenye mitaro
 
Watu wakiwa msibani huku wakijadili mambo mbali mbali. Msiba wa Marehemu Juma Kilowoko 'Sajuki' umewagusa wengi na kuleta simanzi.
 Marehemu Juma Kilowoko anatarajiwa kuzikwa ijumaa saa 5 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA


Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangaraamewatumia salamu za rambirambi, ndugu, jamaa na wasanii wote nchini kufuatia kifo cha msanii Juma Kilowoko (SAJUKI) kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe 02/01/2013 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Taarifa iliyotolewa leo, jijini Dar es salaam ,Wizara ya Habari, Vijana na Utamauni na Michezo imepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha msanii huyo na kuongeza kuwa kifo hicho ni pigo katika tasnia ya filamu hapa nchini.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo Kifo chake ni pengo kubwa kwa Serikali, wadau wa tasnia ya filamu na michezo ya kuigiza nchini kwa ujumla.“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha SAJUKI sina maneno ya kuelezea masikitiko na huzuni nilinayo , kwani kifo chake ni pigo katika tasnia ya filamu za michezo ya kuigiza” alisema Dkt Mukangara.
Dkt. Mukungara amewataka ndugu, jamii na wasanii wote kuwa wavumilivu na watumilivu wakati wote wa msiba na kumuombea marehemu makao mema kwa Mwenyezi Mungu.
Juma Kilowoko (SAJUKI)ni mzaliwa wa mkoa wa Ruvuma. Sajuki alianza kujihusisha na masuala ya maigizo alipojiunga na kikundi cha Kaole na baadaye filamu. Filamu alizocheza ni pamoja na Revenge ya Kampuni ya RJ.
Mwaka 2008 aliamua kuanza kutengeneza kazi zake mwenyewe ambapo filamu yake ya kwanza iitwayo Two Brothers kwa kushirikiana na Shija Deogratious ilitoka. Sajuki baadaye aliamua kuanzisha kampuni yake iitwayo WAJEY Production Company ambapo alitengeneza filamu nyingi zikiwemo Mboni Yangu, Round, Briefcase , Kijacho, Kozopata, Mchanga na Keni, 077( Zero Seven Seven).nk
Sajuki alifanikiwa kucheza michezo ya kuigiza na filamu na wasanii wengi wenye majina hapa nchini. Sajuki amebobea katika Uigizaji, Utayarishaji na Uongozaji wa filamu.
Sajuki alianza kuugua mwaka 2010 na hali ilizidi kudhoofu mwaka 2011,ambapo alikwenda kutibiwa nchini India. Wadau wengi wa tasnia ya filamu walifanikiwa kutoa michango mbalimbali iliyomwezesha Sajuki kupata matibabu yake. Alirudi na kuonekana kapata nafuu kidogo jambo ambalo lilileta matumaini na furaha kwa watanzania; aliporejea tu aliweza kutoa filamu iitwayo Kivuli huku filamu nyingine ikiwa katika hatua ya utengenezaji.
Aidha hali yake ilibadilika jambo lililolazimu alazwe katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili hadi umauti ulipomkuta usiku wa kuamkia tarehe 02/01/2013
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi. AMEN.

Picha na www.elimuboratanzania.blogspot.com

No comments

Powered by Blogger.