ANGALIA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE HAPA


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (MB) leo ametangaza rasmi matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Nne, maarifa na QT.
Mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana yametangazwa. Watahiniwa 240,903 sawa na asilimia 60.6 wamepata sifuri, huku wanafunzi 23,520 tu ambao ni sawa na asilimia 5.16 ndiyo waliofaulu na wengine 103,327 sawa na asilimia 26.02 wamepata daraja la nne.

Akitangaza matokeo hayo , Waziri wa Elimu Dk Shukuru Kawambwa alisema watahiniwa walikuwa 456,137, wa shule wakiwa 397,136 huku wa kujitegemea wakiwa 68,806.
“Matokeo ya mwaka huu yamekuwa mabaya sana, Serikali tunasikitika kutokana na hali hii lakini tuna mipango mbalimbali ya kuhakikisha tunaweza kutatua hili tatizo,” alisema Dk Kawambwa.

Shule bora ni pamoja na St. Francis Girl ya Mbeya, Marian Boys ya Bagamoyo, Feza Boys DSM, Marian Girls Bagamoyo, na Simini ndizo zipo tano bora huku shule nyingine ni Kanosa, Jude, St. Mary.

BOFYA HAPA CHINI KUTIZAMA MATOKEO


No comments

Powered by Blogger.