Mwinyi awaangukia viongozi wa dini
RAIS mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassani Mwinyi amewataka viongozi wa kidini nchini kuihami amani na utulivu inaotishiwa kuvurugwa na misukosuko ya kidini, kisiasa na kijamii inayojitokeza katika maeneo mbalimbali yanchi.
Alhaj Mwinyi alisema hayo wakati
maadhimisho ya sherehe za siku ya uzawa wa Mtume Mohamma (SWA),
yalioandaliwa na Jumuiya ya Khoja Shia Ithnaasheri, kufanyika jijini Dar
es Salaam leo.
Alisema nchi hivi sasa inapita kwenye
misukosuko inayokana na vitendo hivyo na endapo viongozi wa kidini
hawatakuwa makini katika kukemea waumini wao basi huenda nchi ikaingia
kwenye matatizo ambayo hayana slahi kwa nchi.
Alhaj Mwinyi alisema mkiwa viongozi
wadini mnalo jukumu la kila mmoja wenu kutumia elimu na fursa zilizopo
kwa kuwatuliza vijana kutoingia katika vitendo vya uvunjifu wa amani kwa
kisingizio cha dini.
“Tanzania inaongoza kwa kudumisha
amani, utulivu na ustaarabu kwa miaka mingi kama ingekuwa wachezaji
mpira tungesema sisi ni machampioni wa amani katika Bara la
Afrika”alisema Alhaj Mwinyi.
Alisema ni wajibu wa Masheikh hao
kusimamia na kulinda amani na utulivu uendelee kuwepo ili kila muumini
aweze kufanya ibada, kwenda msikitini na kufanya shughuli nyingine za
maendeleo kwa maslahi ya nchi.
Aliongeza kuwa hakuna haja ya
kufikishana mahala kuwa kila mmoja anakuwa na wasiwasi wa maisha yake
kitendo ambacho kinaenda kinyume na mafundisho ya Mtume Mohamad (SWA).
“Tanzania ni nchi kongwe na haikuanza
leo pia ni sawa na gunia ambalo limekusanya watu wengi wa dini
mbalimbali na wasio na dini hivyo ni vema watu wakajenga ustaarabu wa
kuvumiliana”alisema Alhaj Mwinyi.
Alhaj Mwinyi alisema wajibu wa Waislam
ni kuhakikisha wanaishi kwa amani na watu wengine ambao hawajawaingilia
na kutaka kuwafuta katika nchi hii.
Vilevile ieleweke wazi kuwa hakuna
anaweza kumfuta mwenzake katika kile anachokiamini hivyo ni vema kila
mtu akajifunza kumvumilia mwingine.
Alisema kubwa ni kla mmoja kujizuia
kumuingilia mwingine kwenye dini yake, kazi hiyo hakuna mwingine wa
kuifanya bali ni Masheikh hao.
Aliwaasa Masheikh hao kuacha kushabikia mambo madogo ambako ushabibiki ukiendekezwa iko siku unaweza kuvuruga amani ya nchi hii.
Post a Comment