Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Janet Mbene.
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Janet Mbene
ameiomba Serikali kuwatengenezea mazingira mazuri ya kazi wananchi
ili waweze kulipa kodi kwa wakati ambayo itasaidia kuleta maendeleo ya
taifa.
Waziri Mbene aliyasema hayo mwishoni mwa wiki
jijini Dar es Salaam wakati akifanya ziara ya kukagua nyumba 491
zilizopo eneo la Buyuni Kata ya Majohe Wilaya ya Ilala ambazo zimejengwa
na Mradi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF). Alisema
lengo la kujengwa kwa nyumba hizo ni kuwanufaisha wanachama na
wananchi na kwamba Serikali itakapoweka mazingira mazuri ya kazi kwa
wananchi wake wataweza kulipa kodi ambayo itasaidia kuleta maendeleo
katika jamii.
Aliongeza kuwa kila mwananchi ana wajibu wa
kuchangia kodi ambayo itafanya kazi ya kuibua miradi mbalimbali ya
kuleta maendeleo ya jamii ikiwamo ujenzi wa miundombinu ya barabara
“Serikali ifanye jitihada ya kuwawekea mazingira mazuri ya kazi wananchi ili waweze kulipa kodi kwa wakati ambayo itapelekwa kwenye maendeleo ya jamii,” alisema Mbene.
“Serikali ifanye jitihada ya kuwawekea mazingira mazuri ya kazi wananchi ili waweze kulipa kodi kwa wakati ambayo itapelekwa kwenye maendeleo ya jamii,” alisema Mbene.
Pia, aliwataka wanachama wa PSPF kuchangamkia
nyumba hizo waweze kununua au kukopa ili kujikwamua na adha ya kupanga
ikiwamo kupata nyumba bora na za kisasa.
“Nyumba ni nzuri na zitawasaidia wananchi wa
kawaida katika suala la ulipaji wa kodi, wamehakikisha haumizwi katika
ulipaji, ndiyo maana wameamua mtu awe analipa kuanzia miaka 15 hadi
miaka 20,” alisema na kuongeza:
“Nawaomba PSPF kuhakikisha mahitaji muhimu yote
yanayohitajika yanapatikana kama maji, umeme, usafiri na barabara iwekwe
kiwango cha lami itamrahisishia mwananchi atakayehamia kuwa na uhakika
wa usalama wake,” alisema Mbene. Kaimu Mkurugenzi wa PSPF, Adamu
Mayunga alisema wamejipanga kuhakikisha miundombinu ya maji, umeme na
barabara ambavyo ni kilio cha muda mrefu kwa wakazi wa eneo hilo
vinapatikana.
“Tumeshapata mkandarasi wa Manispaa ya Ilala
ambaye amekubali kupeleka greda kwa ajili ya kuchonga barabara na kwa
upande wa maji, Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasco)
ilitujibu itachukua muda mrefu kufikisha mabomba kwenye eneo hili hivyo
tumejipanga kuchimba visima vya maji,” alisema Mayunga.
Alisema nyumba hizo zimejengwa kwa awamu ya kwanza
ambazo zipo kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro Shinyanga, Tabora
na Mtwara hivyo wanachama hao wanatakiwa kununua popote wanakotaka.
Kwa mujibu wa Mayunga, nyumba hizo zitaanza kuuzwa
kwa Sh64 milioni hadi Sh94 milioni kulingana na mahali nyumba
ilipojengwa hiyo gharama ikiwa ni pamoja na kodi ya ongezeko la VAT.
MWANANCHI
MWANANCHI



No comments:
Post a Comment