Rais Chavez arejea Venezuela baada ya matibabu

 Rais wa Venezuela Hugo Chavez, amerejea nyumbani baada ya kupokea matibabu ya saratani nchini Cuba.
Katika ujumbe wake kwa Twitter, Chavez, mwenye umri wa miaka 58, aliwashukuru watu wa Cuba, pamoja na rais Raul na nduguye Fidel Castro.
 
 Mojawapo ya picha zilizotolewa Ijumaa za Rais Chavez akiwa na wanawe

Pia aliwashukuru raia wa Venezuela kwa kuwa naye wakati huu wa matibabu yake.
Amekuwa rais wa miaka 14, na alichaguliwa tena kwa muhula mwingine wa miaka sita Oktoba mwaka jana. Lakini alichelewa kuapishwa kwa sababu ya kuugua.
Bwana Chavez alienda Havana mwezi Disemba kufanyiwa upasuaji kwa mara ya nne tangu agundulike kuugua saratani mwaka 2011.
Wiki jana picha zake baada ya upasuaji zilionyeshwa kwa vyombo vya habari Venezuela.
Aidha Chavez alionekana akitabasamu akiwa na wanawe.
 
Ujumbe wa Rais Chavez ulikuja kupitia Twitter

Chavez aliwatangazia wafuasi wake wa Twitter ambao ni milioni 3.9. Ujumbe wake uliosemekana kuwa mzuri ingawa mfupi.
Hapakuwa na taarifa zozote kuhusu kwa nini na lini alirejea na ikiwa ataweza kuendelea na majukumu yake kama rais.
Badala yake Chavez aliwashukuru viongozi wa Cuba pamoja na wananchi wake na kusema ana imani na madaktari wake.
Ugonjwa anaougua Chavez haujulikani kwa kina lakini unasemekana kuwa mbaya.
Wakati wa matibabu yake, inaanimika alitolewa uvimbe katika sehemu ya fupanyonga yake.
Tangu hapo amepokea matibabu aina ya chemotherapy.
 
 
BBC SWAHILI

No comments

Powered by Blogger.