Dkt. Alberic Kacou awataka watanzania kuacha dhuluma dhidi ya wanawake


Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou akisoma hotuba yake wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika chuo kikuu cha Dar es Salaam ukumbi wa Nkurumah.(Picha na Dewji Blog)

Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu (wa kwanza kulia) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wenzake wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa nchini waliojumuika katika sherehe za kuadhimisha siku ya wamawake duniani iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Ukumbi wa Nkurumah.
Mwakilishi wa UN Women Tanzania Bi. Anna Collins-Falk akizungumzia wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo amesema shirika litahakikisha linafanya kazi kwa ukaribu na serikali ya Tanzania katika kutetea Haki za Wanawake.
Balozi wa Ireland nchini Tanzania Mh. Fionnala Gilsenan aktioa neno la Shukrani kwa wadau, wanafunzi na wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa waliohudhuria sherehe hizo.
Wajumbe wa Chama cha Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA) wakiongozwa na Jokate Mwegelo(wa tatu kushoto)wakijadiliana na kutoa maoni juu ya adha wanazokabiliana nazo wanawake wakati wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Baadhi ya wakuu wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa waliohudhuria maadhimisho hayo.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou (katikati) akiteta jambo na Mwakilishi wa UN Women Tanzania Bi. Anna Collins-Falk wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Mmoja wa wadau wa masuala ya Haki za Wanawake akichangia maoni wakati wa sherehe hizo zilizowakutanisha wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali vya jijini Dar katika Ukumbi wa Nkurumah wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Picha juu na chini Baadhi ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali jijini Dar na wadau wa masuala ya Haki za Wanawake waliohudhuria sherehe hizo.

Baadhi ya Wanfunzi wa vyuo mbalimbali wakijisajili kwenye chama cha vijana cha Umoja wa Mataifa (YUNA) wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ukumbi wa Nkurumah.
It’s a womens Day take care of us…….lol……Wajumbe wa YUNA Tanzania.
Wananchi wa Tanzania na watu wote duniani kwa ujumla wametakiwa kuwa na mikakati endelevu itakayohakikisha inatokomeza uhalifu na dhuluma wanazofanyiwa wanawake yakiwemo matendo ya kubakwa, kupigwa, kunyanyaswa, kunyimwa haki na mengine ya aina hiyo.
Akizungumza wakati akifungua mdahalo juu ya matatizo yanayowakumba wanawake wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani uliofanyika katika ukumbi wa Nkurumah wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dkt. Alberic Kacou amesema wakati umefika sasa kwa dunia kuonyesha kumjali mwanamke kwani katika utekelezaji wa shughuli nyingi za kimaendeleo, uchumi na kijamii mwanamke anahusika.
Ametolea mfano nchini Tanzania takwimu za mwaka 2010 zinaonyesha zaidi ya theluthi moja ya wanawake wote sawa na asilimia 39 wamewahi kukumbana shambulio la kimwili mpaka kufikia miaka 15.
Dkt kacou ameongeza kuwa theluthi mija ya wanawake sawa na asilimia 33 wameshapata mateso ya kufanyiwa vurugu katika kipindi cha miezi 12 iliyopita.
Amesema siku hii ya Wanawake duniani inasherehekewa rasmi kwa sababu kwanza tunatambua kuwa maendeleo, michakato na ustawi kunahitaji ushiriki hai wa kiusawa na kuhusishwa kwa wanawake, pili kwa sababu tunakubali kuwa Amani na Usalama wa Kimataifa unaweza tu kufikiwa kuwa kuwashirikisha wanawake.
Katika mdahalo huo washiriki mbali mbali walipata fursa ya kutaza filamu mbili tofauti zinazoonyesha matatizo yanayowapata wanawake na baada ya hapo walijadiliana na kutoa maoni na mapendekezo kadhaa.
Kauli mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka 2013 ni “ Uelewa wa Masuala ya Jinsia Katika Jamii; Ongeza Kasi

No comments

Powered by Blogger.