MKURUGENZI NA WATENDAJI WAJICHANGANYA

Na John Banda, Dodoma

MKURUGENZI wa manispaa ya Dodoma na watendaji wa kata na kijiji cha Dodoma makuru watupiana mpira wa nani aitishe mkutano wa hadhara ulioshinikizwa na wananchi wa kitongoji cha Njedengwa wanaodai mkutano huo ili wasomewe mapato na matumizi baada ya kutofanyika kwa takribani miaka mitatu sasa.

Hali hiyo imekuja baada ya wananchi wa kitongoji cha njedengwa kuchoka kusubili kwa muda mrefu kuitishwa kwa mkutano wa hadhara ili waweze kusomewa mapato na matumizi na kuamua kumuandikia Barua Mtendaji wa kata zaidi ya mara tatu bila mafanikio na ndipo walipotinga ofisi za Meya na meya kuwaelekeza kwa mkurugenzi aliyeamua mkutano huo kufanyika tar 6 mwezi ujao

Mvutana no huo umekuja kutokana na mkanganyiko uliojitokeza kutokana na hali ya sintofahamu ya Mkurugenzi wa Manispaa Robert Kitimbo na mtendaji wa kata  hiyo ya Makulu Magreth Songoro na wakijiji Namsfu milingo  kushindwa kusema moja kwa moja kuhusu mkutano uliopangwa kufanyika Tar. 6/4/2013 ili kujibu kero mbali mbali za wananchi.

Wakiongea kwa niaba ya wenzao Khatib Sa yuni, Nassol Shomari, Almas Rashid na Matrada Kaaya  walisema waliamua kwenda kutaka msaada kwa Mkurugenzi kutokana na Barua walizomuandikia Mtendaji kata za feb 2/ julai 1. 2012 na mach 19, 2013 hazikujibiwa wala kusainiwa na Mtendaji kata.

Walisema Barua zote walizoandika zilikuwa na madai  mbalimbali yakiwemo ya Kuuzia wageni na kuacha wenyeji zaidi ya viwanja 99 vilivyopimwa na CDA katika eneo hilo la njedengwa korongoni, mradi wa maji ya kitongoji tuliyofadhiliwa kuuziwa  mtu  [kubinafusha] ili auendeshe na kusababisha kitongoji kuingia deni la sh. 618,800.

''Ndugu yangu huyu mtendaji ni tatizo hasa linapokuja swala la maendeleo kitongojini kwetu ona viwanja 99, bomba la maji na kubwa zaidi ni kutoitishwa mkutano kwa kipindi cha miaka 3 ili tujulishwe mapato na matumizi ana yaona madai hayo kisha anakaa kimya bila kumsaidia mwenyekiti ambaye sisi tunajua nafasi yake imepotea kutokana na Tangazo la Serikali na 301 linaloendelea 26-1 kuwa asipoitisha mikutano mitatu mfurulizo nafasi yake itakuwa wazi'', alisema Sayuni

Walisema Barua ya tar 19 mwezi huu waliamua kwa mkurugenzi ambaye baada ya kikao nao kilichowahusisha watendaji aliwaahidi kulifanyia kazi swala hilo na kuwataka waende kwa mtendji siku inayofuata na walipoenda wakajibiwa vibaya kisha kumrudia tena mkurugenzi aliyewambia amuamua kuwena mkutano tar 6.4.2013

Mtendaji wa kata hiyo Magreth Songoro alipotakiwa kutoa ufafanuzi juu ya madai hayo kwanza alisema yeye siyo msemaji japo baadae alisema hivyo ulivyosikia ndivyo ilivyo mkurugenzi atakuja kusikiliza madai yao tar hiyo 6 lakini siyo kutekeleza jambo lolote maana amewapa maelekezo lakini wameshindwa na kuwa wakali japo mtendaji wa mtaa  Namsifu milingo alisema swala hilo kamuulize mkurugenzi.

Mkurugenzi wa manisipaa Rabert Kitimbo alipoulizwa alisema swala hilo ka waulize watendaji wa eneo hilo yeye hawezi kulielezea chochote maana yupo safarini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa Makulu Denis Said alisema mkutano huo utakuwepo na kwamba amemuomba Mkurugenzi waufanye Tar Apr 13. 2013, hata hivyo alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu madai ya viwanja hivyo kuuzwa kwa wageni alisema hichi ni kikundi kidogo cha Watu 7 wahuni wasiyo na kazi achana nao, na kuhusu mapato na matumizi alisema hamna mapato.
 
''hamna mapato wala matumizi nikatoa fedha za mke na watoto wangu nikawasomee mapato na matumizi watu wa njedegwa? nimesema achana nao hao ni wahuni wachache tu wasiojua lolote, Karibu tar 13, nimeongea na Kitimbo atakuja kuwasikiliza na kutakuwa na ulinzi mkali'', alisema.

Hivi karibuni M wenyekiti wa Chama cha mapinduzimkoa wa Dodoma na Mbunge wa Bunge la Africa Mashariki Mhe. Adamu Kimbisa aliwataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kuwabana Watendaji wa kata na vijiji ili waitishe mikutano ya hadhara na kusoma mapato na matumizi ili kuwaondoa wasiwasi wananchi na kuwafanya kujitoa kwa hali na mali kwenye uchangiaji wa maendeleo ya maeneo yao.

No comments

Powered by Blogger.