DIEGO LOPEZ AKIRI UBORA WA MOURINHO, AKIONDOKA HASARA TUPU

Back in town: Jose Mourinho was at Wembley to watch Watford take on Crystal Palace  
ANARUDI ZAKE MJINI: Jose Mourinho alikuwepo Wembley kutazama mechi ya Watford dhidi ya Crystal Palace
In line: Mourinho is expected to take over at Chelsea, who are without Rafa Benitez  
DILI HILO!!: Mourinho anatarajiwa kuichukua Chelsea iiliyomalizana na kocha wa muda Rafa Benitez
Gutting: Diego Lopez laments after Real drew Mourinho's penultimate game at the club  
MBAYA MNO!!: Diego Lopez akijilaumu baada ya Real Madrid kutoa sare ya kufungana mabao 3-3 dhidi ya Real Sociedad jana
Na Baraka Mpenja wa kwa msaada wa Sportsmail.com
Mlinda mlango namba moja kwa sasa wa klabu ya Real Madrid ya Hispania Diego Lopez amesema klabu hiyo kumpoteza kocha mwenye ubora wa hali ya Juu, Mreno Jose Mourinho ni hasara kubwa sana, huku akisisitiza kuwa baadhi ya wachezaji wa timu hiyo nao wamejisikia vibaya.
Mourinho amebakisha mechi moja kuingoza Real Madrid huku kocha wa zamani wa Chelsea ambaye amewapa ubingwa PSG katika ligi ya Ufaransa msimu huu Carlo Anceloti akitajwa kurithi mikoba yake, wakati huo Mourinho akitajwa kurudi Chelsea kurithi mikoba ya Rafa Benitez aliyekuwa kocha wa muda wa klabu hiyo.
Mourinho amekaa misimu mitatu nchini Hispania, lakini msimu wa mwaka huu umekuwa mbaya kwake baada ya kushindwa kutwaa kikombe hata kimoja huku rais wa klabu hiyo Florentino Perez akithibitha kuwa msimu huu ni wa mwisho kwa kcoha huyo mwenye ngebe nyingi zaidi.
Lopez aliyefaidika sana kwa kupata namba katika kikosi cha kwanza baada ya Mourinho kukosa uelewano mzuri na kipa na nahodha wa klabu hiyo Iker Casillas aliongeza kuwa Mourinho ni kocha mwenye haki siku zote.
“Itakuwa hasara kubwa kwa Madrid, Mourinho ni kocha mzuri sana, kwa upande wangu amenifanyia mambo makubwa na kunifanya nijiamini zaidi nikikaa langoni”. Alisema Lopez.

No comments

Powered by Blogger.