HIACE YAMGONGA MWENDESHA BODABODA


  Wakazi wa Ukonga Mazizini Wilayani Ilala jiji la Dar es Salaam wakipita kando ya pikipiki iliyo lala chini baada ya mwendeshaji wake kugonga gari aina Hice mapema asubuhi ya leo kufuatia dereva wa Hice kukata kulia bila ishara.(Picha na Father Kidevu)
 Dereva wa bodaboda shsti ya njano akijadiliana na dereva wa Hice (fulana ya pink) aliyemchomekea ghafla. Dereva huyo wa Hice alichapwa makofi kadhaa na mashuhuda wa ajali hiyo.
 Hii ndo gari iliyowa piga kikumbo.
 Abiria wa bodaboda (mwana dada dera la njano) akiwa na wasamaria wema mara baada ya ajali kutokea nae akiwasilina na marafiki zake kuwa kakoswa koswa na gari.
Dereva wa bodaboda akinyanyua pikipiki yake baada ya kupigwa kikumbo na gari dogo leo katika barabara ya Mandela eneo la Tazara. Abiria wake alishtuka mguu kidogo lakini badae waliendelea na safari.

No comments

Powered by Blogger.