MZEE MANDELA BADO YU MAHUTUTI


Familia ya rais mstaafu Nelson Mandela, imemtembelea hospitalini, mzee Mandela ambaye anasifika kwa vita alivyopigana dhidi ya utawala wa wazungu nchini nAfrika Kusini.
Hali ya Mandela inasemekana kuwa mbaya sana na hakuna habari zaidi zimetolewa kuhusu ikiwa imeimarika tangu ilipotangazwa Jumapili jioni.
Amekuwa akiugua ugonjwa wa mapafu mara kwa mara na hii ni mara ya tatu kwa Mandela kulazwa hospitalini mwaka huu.
Endelea kusoma habari zaidi kwa kubofya hapa chini


Rafiki na jamaa wameendelea kukusanyika katika hospitali alikolazwa Mandela mjini Pretoria kumtakia afya njema mzee Mandela.
Mmoja wa waliomtembelea Mandela , mfanyabiashara Calvin Hugo, aliawachilia huru njiwa weupe, kama heshima yake kwa Mandela anaeyendelea kuugua hospitalini.
Alisema kitendo chake kilikuwa ishara ya, hatua ya Mandela kuikwamua nchi ya Afrika Kusini kutoka kwa mkoloni.
Baadhi ya jamaa zake wamekusanyika nyumbani kijijini eneo la Qunu, kujadili kile wanachosema ni habari muhimu sana.

CHANZO: BBC SWAHILI

No comments

Powered by Blogger.