TIZAMA HAPA MAREHEMU ALBERT MANGWEA ALIVYOAGWA AFRIKA YA KUSINI HAPO JANA


Baada ya kutoka kwenye Mochwari ya serikali ya Hillbrow Johannesburg, mwili wa Ngwea ulihifadhiwa hapa ambako pia msafara wa kwenda kumuaga ndio ulianzia hapa.
 
 Ni zaidi ya Watanzania 50 waliojitokeza kuuaga mwili wa Marehemu Ngwea akiwemo Msanii Bushoke, Mwamvita Makamba, Kinje Ngombale Mwiru pamoja na Watanzania wengine waliokuja kutembea na wanaoishi na kufanya kazi Afrika Kusini.

Marehemu Ngwea alifariki dunia may 28 2013 Johannesburg South Afrika alikokuja kufanya show, ambapo kilikua ni kifo cha ghafla kwa sababu usiku kabla ya kulala aliagana vizuri na Watanzania wenzake kijiweni tena akaahidi kurudi Afrika Kusini baada ya kipindi cha Ramadhani.


Kabla ya kifo chake tayari Ngwea alitakiwa kurudi Tanzania lakini akaahirisha safari yake mara tatu mfululizo ili aendelee kuwepo Afrika Kusini ambako alimwambia Bushoke kwamba amepata mtu wa kumlipia ada hivyo angerudi Afrika Kusini hivi karibuni ili aanze masomo ya muziki.




Gari la Ubalozi wa Tanzania lililotoka Pretoria likiwa na Mwakilishi wa Ubalozi huo, hapa lipo kwenye msafara kuelekea kanisani kuuaga mwili wa Marehemu.



Baadhi ya Watanzania wakiubeba mwili wa Marehemu kuuingiza ili kwenda kuagwa.


Msafara wa magari ya Watanzania mbalimbali.

Josh Kalisa, Habibu Awesi ambae ni mwakilishi wa Ubalozi wa Tanzania Afrika Kusini, Kinje Ngombale Mwiru na Mwamvita Makamba wakiwa nje ya kanisa alikoagwa Marehemu Ngwea.





 











PICHA NA HABARI NI KWA HISANI YA MILLAD AYO

No comments

Powered by Blogger.