JE UNAPIMAJE MAFANIKIO YAKO? JIFUNZE

Namna ambavyo tumeweka fikra na taratibu zetu ni kwaaajili ya mazuri na mabaya *lakini mabaya hasa* pale tunapojilinganisha na watu wengine.
Unaelewa ninachokiongelea hapa? Mara nyingi tunajitahidi kufanya kwa kumtazama yule aliye karibu nawe na kuona yuko wapi na mimi niwe wapi. Hivyo tunajaribu kutafuta wapi ninaweza kutengeneza hela zaidi, ninunue gari kama wengine au kukaa kwenye nyumba zuri kama wengine. Nataka niwe mwembamba kama fulani au niwe mnene kiasi na hata inapokuja kwenye biashara tunajaribu kufanya hivyo hivyo.
Unaomba nikuondolee shaka katika mada hii, si kwamba hutakiwi kujilinganisha na watu wengine, unahitaji kupata akili hapa, unatakiwa kujua ninaongelea nini katika makala hii. Wewe kufanya zaidi ya wengine au kupata changamoto kutoka kwa wengine ni nzuri zaidi. Au kuwa na biashara inayouza zaidi ya wengine ni jambo la kuvutia pia. Lakini kitu ambacho ninakijua zaidi ni kwamba, “Kujilinganisha ni kwa wale ambao hawana mategemeo yao binafsi” kitu gani kilikuvutia kuanza hiyo biashara na malengo yako yalikuwa ni nini?. Jenga bidhaa yako na hicho ndicho cha muhimu, mambo ya kukumbuka ni kama haya.
Kaa chini jiulize , Je ninapima mafanikio kwa namna gani? Kabla ya kujibu naomba nikupe dondoo chache:

ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

  • Je una shauku na hamasa ya kile unachokifanya ?
  • Umeleta utofauti gani? – hata kama ni kidogo kila siku ?
  • Je wateja wako wanafurahia huduma au bidhaa yako baada ya kuitumia?
  • Je una timu ya watu wanaokuunga mkono na kukupongeza unapofanya vizuri? au kukushauri unapofanya vibaya?
  • Je kazi yako ni kofia unayovaa kila siku?
Utagundua majibu ya maswali hayo hayapatikani kwa kuwaangalia watu wengine, unahitaji kuyajibu kutoka kwenye moyo wako mwenyewe na maisha yako mwenyewe au kwa ajili ya kampuni yako mwenyewe. Ndipo utaanza kujiuliza kuhusu fedha, watu kukutambua na umaarufu.
Ukweli ni kwamba ukijenga biashara yako kwaajili ya fedha, kujulikana na umaarufu, mambo mawili yanaweza kutokea;
  • Hautashinda. Hautakuwa na mali au fedha ya kutosha au hata umaarufu utaukosa. haijalishi utatengeneza kiasi gani lazima utakuta kuna mtu amekuzidi.
  • Umaarufu na kujulikana kutakwisha na utabaki mtu wa kawaida. Hakuna kitakachokufanya uendelee vizuri kwenye maisha yako na biashara yako kama kuwa na shauku na hamasa ya kile unachokifanya.
Na kitu cha mwisho ni kwamba bidhaa nzuri ni wateja, kujilinganisha ni matatizo yako binafsi katika fikra haitatokea ulingane na mtu yeyote kwa sababu haijawahi kutokea kwenye maisha ya kawaida. Unapokuwa na mawazo kwamba wewe ni bora kuliko wengine haina maana kama wateja wako hawasemi hivyo. Na kama unataka wateja wako waseme hivyo zingatia hizo dondoo hapo juu.

Upande wako ukoje? Je mafanikio kwako ni nini?

No comments

Powered by Blogger.