LEO NI KUMBUKUMBU YA MWAKA MMOJA TANGU BI KIDUDE AFARIKI DUNIA


Leo April 17, kifo cha aliyekuwa mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Taarab nchini, Fatuma binti Baraka maarufu kama Bi. Kidude kimetiza mwaka mmoja.
Bi. Kidude alifariki kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya sukari na uvimbe kwenye kongosho.
“Kwa ufupi alilazwa kipindi kirefu na baadaye akatolewa, lakini baadaye akaja kuendelea kuumwa tena tukampeleka hospitali tukawa tunampeleka kwenda na kurudi hapa juzi akaanza kuzidiwa tena tukampeleka hospitali moja inaitwa Keeni (???) Kwaajili ya matibabu zaidi na drip na vitu vingine lakini baadaye baada ya siku ya tatu mwenyezi Mungu akachukua roho yake,” mjukuu wa Bi Kidude aitwae Omar alisema siku kama ya leo mwaka jana.
Msiba wa marehemu Bi. Kidude haukuwa wa Tanzania tu bali ni wa dunia nzima. Mashirika makubwa ya utangazaji duniani yaliwahi kufanya naye mahojiano kutaka kupata historia yake ya kuvutia. Mwaka jana kituo cha CNN kilimtembelea Bi. Kidude nyumbani kwake Zanzibar na kumhoji. Mtangazaji wa CNN aliyefanya naye mahojiano kwenye kipindi cha Inside Africa, Errol Barnet ni miongoni mwa watu waliosikitishwa na msiba huo.

No comments

Powered by Blogger.