MAASKARI NCHINI CHINA WAKAMATA MAKOMBE FEKI ZAIDI YA 1000 YA KOMBE LA DUNIA
Wakati ziara ya dunia ya kikombe halisi cha kombe la dunia ikiendelea
kabla ya kukabidhiwa kwa mmiliki wake mpya ambaye ni mshindi wa mwaka
huu huko Brazil, maafisa wa China wamekamata makombe feki ya kombe la
dunia zaidi ya 1,000, yaliyokuwa yamedhamiriwa kuuzwa katika kona
mbalimbali za dunia.
Maaskari wakitazama makombe feki
Ikiwa zimebaki siku chache kabla kombe la
dunia 2014 halijaanza kutimua nyasi huko Brazil , maafisa wa forodha wa
China wamekamata makombe hayo ya dhahabu 1,020 huko katika mji wa Yiwu
yakiwa tayari kusafirishwa kuelekea Libya kuuzwa, na kabla ya hapo
makombe mengine feki 1,008 yalikamatwa.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Kwa kuyatazama makombe hayo feki yanafanana sana na kombe halisi la dunia.
Kombe halisi la dunia
Kombe halisi la dunia pia lilikuja Tanzania mwishoni mwa mwaka jana 2013.
Source: Mail Online
Post a Comment