MAMBO SITA(6) AMBAYO HUPASWI KUYAAMINI KATIKA SUALA LA UONGOZI


Tunaishi katika dunia ambayo inapenda majibu rahisi na ya haraka. Wakati mwingine viongozi wamekuwa wakija na mawazo ambayo si sahihi ila watu wafuata. Wakati nikiwa mdogo nilikuwa naamini vitu vingi kuhusu uongozi na baadaye kuja kugundua ni habari tu za mtaani na si ukweli kuhusu uongozi.
Soma mambo haya ambayo yameenea sana lakini hayana ukweli ndani yake kuhusu uongozi: 

1. Mameneja/Mabosi wote ni Viongozi: Ukweli: Mameneja/Mabosi wengine ni viongozi na wengine sio viongozi.Kitengo cha utendaji ni kipengele kidogo na mojawapo katika uongozi. Mameneja ni wazuri katika kutengeneza, kuendesha na kusimamia mfumo mzima wa kazi ambavyo unatakiwa ufanyike. Wao huajiri watu, lakini hawawezi kumtoa mtu ili awe bora na kulichukua shirika kwenda viwango vingine, kwa sababu wao hawaongozi ila wanasimamia.
Uongozi sikuzote unahusisha mabadiliko, uboreshaji na ukuaji.

2. Viongozi wengine ni wakuzaliwa: Ukweli: Hata kama mtu amezaliwa kama anaweza kuongoza lazima ajifunze ujuzi na mbinu za kuongoza.
Mtoto au kijana anaweza kuwa anajua kucheza mpira, ili aweze kucheza vizuri anatakiwa kufunzwa namna mbalimbali za kuweza kucheza vizuri zaidi.
Kwa wengine wanaweza kuwa na uwezo wa kuongoza tokea akiwa mdogo lakini lazima aendelezwe kwenye tabia,utu na hulka yake na sio kwasababu alizaliwa anaweza kuongoza.

ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


3. Viongozi siku zote wana majibu sahihi: Ukweli: Viongozi huuliza maswali sahihi na wanajua wapi watapata majibu. Kama watu wanakuja kwako kila wakati kwa kutafuta majibu, wewe una uwezo mkubwa wa kufikiri. Ila kama kila mtu anauliza swali hilo hilo kwako inamaanisha wewe sio mbunifu. Unapokuwa huulizi maswali na unashindwa kutafuta ufumbuzi wa mambo yanavyotokea utajikuta unajibu na kufikiri kama zamani au kwa lugha nyingine huna jipya katika majibu yako.

4. Unahitaji cheo ili uongoze: Ukweli: Kuongoza unahitaji kujua ni wakati gani uongoze kitu gani na ufanyaje. Uongozi ni namna ya kuhakikisha mambo yanakwenda vizuri na kwa ubora pale pale ulipo hailjalishi una cheo au hauna cheo. Taasisi bora duniani humsaidia kila mtu katika taasisi hiyo kuwa na uwezo wa kuongoza na kuchukua majukumu kwa kile wanachofanya ili kuleta matokeo bora.

5. Viongozi wana mwelekeo /msimamo katika ufanyaji wa mambo: Ukweli: Viongozi hutengeneza na hushirikisha mwelekeo/msimamo kwa watu wengine. Kama timu yenu au taasisi yenu haina mwelekeo haijalishi wewe una mwelekeo gani, hamtaweza kufanya kinacho eleweka. Mameneja huwa na mwelekeo ila viongozi hutengeneza na hushirikisha huo mwelekeo kwa watu wengine ili wasitumie mali ghafi vibaya kwa kufanya mambo ambayo hayahusiani na dira ya taasisi hiyo.
Kuwa na mwelekeo/msimamo ni wajibu binafsi na inahitaji kijitunza na kujiheshimu.Ila unapotengeneza mweleko au msimamo ni kitendo cha wewe kuwashirikisha wengine ajenda kwaajili ya kazi fulani.

6. Kila mtu anaweza kuongoza: Ukweli: Hakuna anayeweza kuongoza kama hana hamu ya kuongoza.
Huwezi kumfanya mtu aongoze, ni kama kumpeleka punda mtoni. Unaweza ukafika mtoni na punda akagoma kunywa maji, vivyo hivyo kwenye uongozi unaweza kukawa na jambo linaendelea n kila mtu anasubiri mtu mwingine atoe mwongozo. Ile hamu ya kuongoza na kuchukua hatua hiyo ni dalili nzuri katika uongozi. Ukijua ukweli kuhusu uongozi ni kitu kitakufanya uwe bora kwa namna unavyoongoza.

CHANZO: BONGO 5

No comments

Powered by Blogger.