PICHA: BAADHI YA WAJUMBE WAREJEA BUNGENI, MJADALA WA KATIBA WAENDELEA


 Mjumbe wa Bunge la Katiba, Mhe.  Ezekiel Oluoch akiingia jana kwenye  kikao cha Bunge Maalum la Katiba  mjini Dodoma. Mhe. Uluoch, ambaye pia ni naibu katibu mkuu wa Chama cha Walimu (CWT), ni mmoja wa wachangia mada wakubwa aliyejipatia umaarufu mkubwa mjengoni.
Mhe. Uluoch akisimama kutoa ufafanuzi kuwa yeye hana kundi bungeni humo.
  Wakati bunge Maalum la Katiba linaendelea na kikao leo, baadhi ya wajumbe waliokuwa wanasemekana kuwa ni wanachama wa umoja wa kinachoitwa katiba ya wananchi (UKAWA) wamejitokeza na baadhi yao kukanusha kuunga mkono umoja huo. 

 ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


Mmoja wao ni Mhe Ezekiel Oluoch ambaye alikuwa anadaiwa kuwa miongoni mwa WANA UKAWA aliingia Bungeni jana na kukana kuhusika na umoja huo na kuongeza kuwa yeye hana kundi lolote ndani ya bunge, na kwamba ataendelea na kazi ya aliyoteuliwa kuifanya. 
Mjumbe ambaye ni mwakilishi wa wakulima Mhe.Hamisi Damumbaya akichangia  pamoja na kuwataka UKAWA kurejea kwenye mchakato wa katiba mpya. Amewasifu  viongozi wa dini kwa kutumia mahubiri  kuelimisha wananchi kuhusu katiba wakati wa kipindi cha ibada za Pasaka nchini kote.
 Mwenyekiti  wa Bunge Maalum la KAtiba Mhe.Samwel sitta akiliambia Bunge jana kuwa pamoja na UKAWA kuondoka koramu ya wabunge walio ndani ya ukumbi imetimia kwa hiyo mchakato wa katiba mpya utaendelea kama kawaida.
Hii inafuatia kikundi kinachojiita umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) kususia Bunge wiki iliyopita, na baada ya baadhi yao kurudi na kuendelea na bunge kama kawaida.
Wanaoendelea na bunge wengi ni kutoka kundi la wateule 201 na baadhi ya vyama vya upinzani ambao mwanzo walionekana kuunga mkono UKAWA.
Na Deusdedit Moshi Mtendaji Mkuu wa 
Photo Solutions Wawakilishi wa Michuzi Blog Kanda ya Kati.
Mwenyekiti wa Kamati namba tano ambaye anatoka chama cha wananchi CUF Mhe.Hamad Rashid akichangia mjadala jana na kuliaminisha bunge kuwa pamoja na wanaojiita wana ukawa kutaka mfumo wa serikali tatu yeye anaamini mfumo wa serikali mbili na kuwashangaa wenzake kwa kuwa vigeugeu na kwamba maridhiano yatapatikana ndani ya bunge na si nje ya bunge.

No comments

Powered by Blogger.