UPDATES: MELI YA MIZIGO YAZAMA KWENYE ZIWA LA VICTORIA


Watu 10 wamenusurika kufa maji katika ziwa Victoria baada ya meli ya mizigo Fb Matara kupinduka na kuzama ikiwa na shehena ya sukari tani 280 zilizonunuliwa katika kiwanda cha sukari Kagera wakati ikitoka Bukoba kwenda jijini Mwanza.
Meli hiyo inayomilikiwa na kampuni ya Mkombozi fishing and marine transport limited, imezama ikiwa na magunia 5600 ya sukari sawa na tani 280, mali ya mfanyabiashara wa jijini Mwanza aitwaye V.h. Shah, ambapo mkurugenzi wa kampuni hiyo Gitano Chacha Munanka ameeleza kwamba meli hiyo imezama ikiwa katikati ya visiwa vya Kerebe na Lukolu majira ya saa 10.30 usiku na kuongeza kwamba hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa kufuatia tukio hilo.
ITV imeshuhudia meli hiyo ikiwa imepinduka huku juhudi za wafanyakazi wa kampuni hiyo kuipundua zikiwa zinaendelea bila mafanikio, huku baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wakisema chanzo cha meli hiyo kuzama ni kutokana na dhoruba kali ambapo wametoa ushauri kwa wamiliki wa vyombo vya majini kuzingatia utabiri unaotolewa na mamlaka ya hali ya hewa nchini ili kuepusha maafa.

 ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

 
Meli hii inayoonekana pichani ni mfano wa meli iliyozama,ambayo ilianza safari yake ya kutoka Bukoba majira ya saa 7 mchana, ikiwa inaendeshwa na kapteni Erick Lasana – mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu Sumatra kanda ya ziwa, umethibitisha kuzama kwa meli hiyo yenye uwezo wa kubeba tani 280 za mizigo na abiria 100.

CHANZO: ITV TANZANIA


No comments

Powered by Blogger.