AJALI: WATU WATATU WANUSURIKA KIFO BAADA YA GARI KUINGIA MTARONI ENEO LA KIJITONYAMA, JIJINI DAR

 Mchina aliyekuwamo kwenye gari akizungumza kwa simu, pembeni yake ni askari wa usalama barabarani.
Watu watatu akiwemo raia wa China na dereva ambaye ni mtanzania wamenusurika kufa katika ajali iliyotokea maeneo ya Millennium Tower, Kijitonyama jijini Dar es Salaam ikihusisha gari ndogo aina ya Opa.
 Dereva wa Opa ambaye hakufahamika jina lake mara moja.
Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni gari la zimamoto lililokuwa linatokea njia ya Mikocheni kuingia barabara kubwa.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

 Watu wakishuhudia gari likitolewa mtaroni.
“Gari la fire lilikuwa kasi sana huku likipiga king’ora, kwa hiyo kujihami dereva mwenye Opa akajikuta ameingia mtaroni, tunashukuru hakuna aliyeumia,’’ alisema Robert.



Aidha mtu mwingine aliyenusurika katika ajali hiyo ni Abdukarim ambaye alikuwa ndani ya mtaro huo akisafisha. Askari wa usalama barabarani alifika eneo la tukio huku break down likianza kuitoa gari hiyo mtaroni.
 Gari la break down likivuta Opa iliyoingia mtaroni.
Aliyenusurika katika ajali hiyo, Abdukarim akiwa pembeni akitafakali.

No comments

Powered by Blogger.