BREAKING NEWS: ALIYEKUWA MKURUGENZI WA TBS BWANA CHARLES IKEREGE AHUKUMIWA KWENDA JELA


Na Mwene Said

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Nchini (TBS), Charles Ekelege amehukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwenda jela miaka mitatu na kuilipa serikali Dola 42,543 za Kimarekani, baada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka kwa kutoa asilimia 50.

Kadhalika, Ekelege anadaiwa kutoa asilimi hiyo ya  punguzo la tozo ya utawala kwa Kampuni mbili  Kampuni ya Jaffar Mohamed Ali Garage na Kampuni Quality Motors na kulisababishia shirika hilo hasara ya dola hizo.

Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi  Augustina Mmbando baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili na mahakama yake kumuona mshtakiwa bila kuacha shaka ana hatia.

Hakimu alisema ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri ulieleza mahakama kwamba mshtakiwa kupitia wadhifa wake alifanya maamuzi bila kinyume na sheria za TBS zinazomwelekeza kuwasilisha masuala yote ya kiutendaji kwenye Bodi ya Wakurugenzi.

Alisema kitendo cha kutoa msamaha kwa kampuni hizo bila kuacha shaka moja kwa moja mahakama imeona alitumia madaraka yake vibaya.

“Kwa upande wa  shitaka la pili, kiongozi yeyote katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anapokuwa madarakani ni kwa ajili ya maslahi ya taifa, lakini mshtakiwa alikosa uzalendo na kutumia madaraka yake vibaya kuhujumu uchumi” alifafanua hakimu kuhusu ushahidi wa Jamhuri.

 “Mahakama inamuona mshtakiwa ana hatia katika kosa hili la pili la kujumu uchumi … pia mshtakiwa amesababisha watanzania waliompa dhamana kukosa kula keki ya taifa lao kwa kujinufaisha yeye binafsi” alisema hakimu huyo na kuongeza kuwa.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA  CHINI


“Katika ushahidi uliotolewa na mshtakiwa alikiri kufanya maamuzi bila kupata baraka na kibali cha Bodi ya Wakurugenzi na kwamba aliidanyanya mahakama” alisema Hakimu Mmbando.

Akifafanua zaidi alisema mshtakiwa alidai kuwa katika kutoa maamuzi pinguzo kwa kampuni hizo alishirikisha menejimenti na kwamba shirika lilikuwa na utaratibu wa kufanya kikao kila siku asubuhi.

Hata hivyo, shahidi wa pili wa utetezi Thomas Mlugulu alishindwa kuieleza mahakama wajumbe waliokuwa wakihudhuria kikao cha cha asubuhi cha shirika kwa kila siku zaidi ya kumtaja Betwel Matemba ambaye alishakufa na hawezi kufika mahakamani.

Alisema ushahidi wa utetezi ulikuwa dhaifu kushindwa kukanusha ushahidi wa Jamhuri ulioweza kuithibitishia mahakama ukweli kuhusu mashitaka yanayomkabili Ekerege.

Hakimu alisema mahakama pia inamtia hatia mshtakiwa kwa shitaka la tatu la kuisababishia serikali hasara ya dola hizo na kuwasababishia watanzania kukosa kula keki ya taifa lao.

Hakimu Mmbando alitoa nafasi kwa mawakili wa pande zote mbili kutoa hoja kabla ya kusoma adhabu.

Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Janeth Machulya, alidai kuwa kulingana na makosa aliyotiwa hatiani mshtakiwa kwamba alipewa dhamana na rais pamoja na watanzania lakini aameshindwa kuwa mzalendo.

“Kwa kuwa mshtakiwa ameshindwa kuwa mzalendo kwa mamlaka aliyopewa na wananchi, tunaomba mahakama itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa vigogo wote wanaopewa madakara na kuyatumia vibaya,” alidai na kuongeza.

“Mheshimiwa kwa kosa la uhujumu uchumi mahakama izingatiee utoaji wa adhabu kulingana na sheria ya kosa hilo inavyoelekeza” alisema Machulya aliyeongoza mashahidi wa Jamhuri katika kesi hiyo na mahakama kumtia hatiani kigogo huyo.
Wakili wa utetezi Majura Magafu alidai kuwa mahakama imuonee huruma mshtakiwa kwa sababu ana familia inamtegemea.

Pia, wakili huyo alidai kuwa mshtakiwa anajutia makosa aliyofanya na kwamba  akipewa nafasi hawezi kurudia.
Hukumu hiyo iliyoanza kusomwa saa 6:20 mchana hadi saa 8:10 hakimu aliahirisha kwa nusu saa kabla ya kusoma adhabu.

Saa 8:49 mahakama iliyoketi chini Hakimu Mmbando ilianza shughuli zake.

Akisoma adhabu hiyo, hakimu alisema Viongozi wote wa serikali wako juu kwa ajili ya kulinda maslahi ya taifa ili kulinda na kuangalia nchi na mali zake, siyo kuongoza kwa matakwa ya kiongozi husika.

“Mshtakiwa unastahili kuhukumiwa ili kuwa mfano kwa viongozi wengine wanaochezea keki ya taifa hili kwa manufaa yao binafsi… unakwenda jela mwaka mmoja kwa kosa la kwanza, mwaka mmoja kwa kosa la pili na mmoja mwingine kwa kosa la tatu na ailipe serikali fedha alizoisababisha hasara” alisema Hakimu Mmbando.

Baada ya hukumu kusomwa;
Mshtakiwa alianza kububujikwa na machozi huku watu wanaodaiwa kuwa familia yake wakiangua vilio kwa sauti wakati mpendwa wao akiwa chini ya ulinzi tayari kwenda gerezani kuanza kutumikia kifungo.
Watu mbalimbali waliokuwa katika viunga vya mahakama hiyo walimzunguka mshtakiwa huyo huku kila mmoja akisema lwake’jamani jela ni jela’ wengine ‘tatizo hizo fedha alizoambiwa alipe anazo au alishakula zote’ walisikika wakizunguma.

Mapema Mwaka 2012, aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Cyril Chami aliondolewa katika wadhifa huo kutokana na kashfa ya kutoa punguzo la tozo na baadaye Mei 21, mwaka 2012, mshtakiwa alisimamishwa kazi kama Mkurugenzi wa TBS ili kupisha uchunguzi na hatimaye jana kuhumiwa.

Katika kesi ya msingi, Ekelege anadaiwa kuwa kufanya matumizi mabaya ya madaraka kwa kutoa asilimia 50 ya punguzo la tozo ya utawala kwa kampuni hizo mbili.

Pia, ilidaiwa kuwa Machi 28, mwaka 2008 na Agosti 7, mwaka 2009, katika ofisi za TBS zilizopo wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, kwa nia ovu Ekerege alitumia madaraka yake vibaya.

Ilidaiwa kuwa mshtakiwa huyo alitumia madaraka yake vibaya kwa kutoa punguzo la asilimia 50 ya ada ya utawala kwa kampuni hizo bila idhini ya baraza la utendaji la TBS kinyume cha sheria namba 2 kifungu kidogo cha (3) ya TBS ya mwaka 2005.

Ilidaiwa kuwa kitendo hicho kiliziongezea kampuni hizo faida ya Dola 42,543 za Kimarekani sawa na (kwa wakati huo) Sh. Milioni 68,068,800.

Upande huo wa Jamhuri ulidaiwa shitaka la pili, katika tarehe na mahali pa tukio la kwanza, mshtakiwa alilisababishia shirika kupata hasara ya fedha hizo.

CHANZO: MICHUZI BLOG

No comments

Powered by Blogger.