JE, UNALIFAHAMU TATIZO LA FANGASI WA MIGUUNI LINATOKANA NA NINI, NA TATIZO LA KUNUKA MIGUU? HEBU TUELIMISHANE JAPO KWA UFUPI.

Fangasi wa miguuni wanaweza kumpata mtu yeyote endapo tu mazingira yafuatayo yatakuwepo:
1.Unatembea bila viatu sehemu ambayo ina aina hii ya fangasi.

2.Ikiwa miguu iko katika joto na inatoa jasho wakati umevaa viatu.
Wanachofanya fangasi hawa ni kutafuna seli za ngozi ya zamani ya miguu. Japo huwapata zaidi watoto kwa kuwa hawako makini na miguu yao na pia aina ya michezo wanayocheza lakini wakubwa pia ni wahanga wa hili.

ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Hebu tuangalie dalili zinazoweza kuashiria kwamba miguu yako inashambuliwa na aina hii ya fangasi:

1.Vinundu vidogo vidogo miguuni

2.Mipasuko, malengelenge, na kubanduka kwa ngozi kati ya uwazi wa vidole.

3.Wekundu na alama katika nyayo za miguu.

4.Ngozi kati ya vidole kutoa harufu isiyo nzuri.

5.Vipele ambavyo vinasambaa kuelekea ndani ya ngozi ilipasuka.

6.Kutoka na ngozi nyembamba endapo utakuna sehemu za miguu.

Fangasi hawa wanaweza kuendelea na uharibifu wao mpaka eneo lingine la miguu, kama kucha na kuziharibu kabisa. Kuna watu huwa wanaugua mara moja tu na kufanikiwa kulimaliza, lakini wengine limekuwa ndio uwanja wao wa nyumbani.

Akipona leo, kesho kutwa linarudi tena na yeye anachukulia kawaida tu huku akiwapa tabu watu wanaomzunguka. Kwani kuna kipindi linaambatana na bakteria ambao wanatoa harufu mbaya sana miguuni. Tabu huja pale anapovua viatu mbele za watu, watu walio karibu naye wanakuwa kwenye janga lisilosemeka, na muda mwengine kumwambia inahitaji ujasiri sana.
Sasa  tuangalie njia amabazo tunaweza kuzitumia  kuondokana na tatizo hili:
1.Osha miguu yako vizuri kila siku.

2.Kausha miguu na kitambaa kikavu hasa kati ya vidole ambako maji ndio hujificha huko.

3.Epuka kuvaa viatu vinavyokubana na kutotoa nafasi miguu yako kupumua.

4.Vaa viatu vya wazi unapotembea maeneo kama bafu linalotumiwa na watu wengi au maeneo ya kufanyia mazoezi.

5.Tumia soksi ambazo zinanyonya enyevu, kama zilizotengenezwa kwa pamba.

6.Badilisha soksi kila mara na usipende kurudia rudia.

7.Usishirikiane kuvaa viatu na mtu mwengine.

8.Safisha vizuri eneo la kuogea pindi unapomaliza kulitumia.

No comments

Powered by Blogger.