MUHIMU KWA WAZAZI: YATAMBUE MAKOSA AMBAYO WAZAZI WA KITANZANIA HUYAFANYA KWENYE MALEZI YA WATOTO WAO

Una habari kwamba  Brooklyn Beckham (15), mtoto wa bilionea na mwanasoka wa zamani maarufu duniani David Beckam anafanya kazi mgahawani? Tena analipwa euro 2.6 kwa saa Yaani Sh 6000/= za kitanzania.

 Je baba yake asingeweza kumpa mshahara mara 10 ya huo tena kwa kukaa  tu ndani?. Utakubaliana na mimi kwamba wazazi wa sasa wanawekeza zaidi katika maisha ya watoto wao kuliko kizazi chochote kile kilichowahi kutokea! Pengine ni mabadiliko ya kimaisha, lakini Je, hiki tunachokiita “malezi ya kisasa” Kinaweza kuleta Madhara gani Baadae? Je, tunatengeneza taifa la namna gani baadae? Nia yangu sio kumnyooshea mtu kidole bali kujaribu kujenga uelewa zaidi katika jamii yafuatayo ni baadhi ya mambo kumi wazazi hukosea katika malezi:

1.Tunalea  “Mtoto tunayemtaka”  sio  “mtoto tuliyenae”
Wazazi wengi  hulea watoto wao wakitaka kuwachagulia aina Fulani ya maisha bila kujali mtoto walienae  anaweza vitu ganina na kupenda nini. Badala yake kila mzazi huamini mwanae atakua na tabia kama za kwake na pengine atakua na akili na uwezo zaidi au hulazimisha mwanae awe na kipaji Fulani eti tu kawa kuwa mzazi ana kipaji/kalama hiyo! Kumbe ingekuwa hivyo basi tusingehangaika kutafuta viongozi, wanasoka au wasanii bora kwani tungewatumia watoto wao tu!

2. Kusahau Kuwa Vitendo vyetu (wazazi) vinaongea kwa sauti kubwa zaidi ya maneno/ nasaha zetu
Unaishi vipi na majirani zako? Je unaishi vipi na mwenzi wako hapo ndani?  Unaishi vipi na wageni? Kama ulikuwa hujajua, basi tambua kwamba mwalimu wa kwanza wa mtoto ni mzazi, mtoto yeyote anapokuwa hupenda kuwa kama baba/mama yake. Je anayoyaona unayafanya ni sawa na unachomwambia afanye?

ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

3. Kudharau Tabia za mwanzo za mtoto
Tabia yoyote anayokuonyesha mwanao katika umri mdogo, ndiyo hiyo atakayoionyesha akiwa na miaka 30!. Kama anatabia ya ubinafsi, ambayo pengine kajifunza kwa mzazi mmojawapo, shuleni nk, basi usitegemee maajabu kuwa mtoto atabadilika na kutumia neno “ni utoto”. Zijue tabia Za mwanzo za mwanao, mbadilishe mapema iwezekanavyo (kama ni mbaya) kwani akizoea itakuwa sehemu ya maisha yake na itakuwa “vita” kutaka kumbadilisha akiwa na umri mkubwa zaidi.

4. Kulea Kwa mashindano
Mara kadhaa utasikia watu wakisema mtoto wa mzee Fulani ana afya eti tu kutokana na unene uliopitiliza. Au utasikia Shule Fulani ndio bora kwa kuwa tu wana ada kubwa na wengine hutaka watoto wao wawe hivyo na kuenda huko ili tu kupata heshima kumbe ni hatari kwa mwanao ama unafanya mambo yaliyojuu ya uwezo wako unaishia kujinyima Kupita kiasi matokeo yake hutaweza kutimiza mahitaji mengine muhimu kwa familia yako!

5. Kusahau Ibada
Kila mtoto huhitaji mazingira ya kuchagua ni mtu gani katika maisha angependa kuwa kama yeye (needs variety of role models)  na hakuna sehemu salama kwa makuzi ya mwanao kama nyumba za ibada kwani licha ya kufundishwa dini, huko atafundishwa mabaya ni yapi na mazuri ni yapi pia. Mfano Utafiti unaonyesha kuwa mtoto akiambiwa ukitenda baya Fulani utachomwa moto ataacha mara moja tofauti na mtu mzima. Hivyo hata kama mzazi huna tabia ya kwenda kanisani/msikitini basi jitahidi mwanao aende.

6. Kuamini watoto wetu hawana makosa (wamekamilika)
Tatizo kubwa ninalolisikia kutoka kwa walimu, washauri, wasichana wa kazi,  au walezi wengine wa watoto kwenye mashule na majumban  ni kwamba wazazi wengi hawapendi kusikia mambo hasi (ubaya)  yanayohusu watoto wao. Wengi hudai watoto wao hawako hivyo, wakisahau kuwa wao wametingwa na majukumu mbalimbali na hawajui maendeleo yoyote ya mtoto!
Wa kwanza kulaumiwa huwa ni mlezi huyo na mzazi hukaa upande wa mtoto. Matokeo yake mtoto hatamsikiliza mlezi wake tena kwani anajua mzazi yuko upande wake!

7.Kutomsikiliza kabisa/ Kumsikiliza Kupita Kiasi

8.Kutowapa nafasi ya kucheza Utotoni
Ulishawahi  kurudi  nyumbani ukakuta kuta zako zote za nyumba  zimechorwa vipepeo, midoli na kubandikwa stika mbalimbali ? Je, ulichukua hatua gani? Ukweli ni kwamba hiyo ni moja ya Baraka uliyopewa kushirikiana maisha na viumbe hawa wadogo.  Siku moja hakutakuwa na michoro ukutani, wala midoli kitandani kwako, hutasikia kelele za aina yoyote  na utajiona mpweke watakapokwenda kuanzisha familia zao.
Tunahitaji kuwapa watoto muda mwingi wa kucheza na wenzao kwani hii huwapa nafasi ya kuzijua kalama na vipaji vyao. Pia huwapa watoto hali ya kujiamini na kufanya maamuzi.

9.Kutokula pamoja na watoto wetu

10.Wazazi Kutokua Kitu Kimoja
Kama nilivyosema hapo juu, hakuna mwalimu wa muhimu kama mzazi, na mtoto anahitaji malezi ya pande zote pili ikizingatiwa nae atakuwa mzazi siku moja. Wengi wa wazazi huangalia zaidi namna ya kuwatimizia mahitaji watoto nakusahau maisha yao binafsi.

No comments

Powered by Blogger.