TANI 7 ZA VIPODOZI FEKI ZATEKETEZWA MKOANI TANGA

Tani 7 za vipodozi vinavyodaiwa kuwa na viambata vyenye sumu vimeteketezwa kwa moto katika dampo la mwang'ombe lililopo jijini Tanga kufuatia wakaguzi wa idara ya afya kufanya msako mkali na wa kushtukiza. Katika baadhi ya maduka kisha kubaini kuuzwa kwa bidhaa hizo ambazo inadaiwa kuwa zimekuwa zikisababisha maradhi kwa watumiaji ikiwa ni pamoja na saratani ya ngozi.
Mratibu anayesimamia masuala ya chakula na dawa wa halmashauri ya jiji la Tanga Bi. Alis Maungu amesema shehena hiyo ya vipodozi wameiteketeza ili kusaidia kupunguza madhara kwa watumiaji kwa sababu serikali imepiga marufuku bidhaa hizo kuuzwa madukani lakini baadhi ya wafanyabiashara bado wamekuwa wakikaidi agizo hilo.
Amewatadharisha watumiaji hasa wanawake ambao wanaopenda kubadilisha ngozi zao kuwa nyeupe kuchukua tahadhari kwa sababu madhara ya vipodozi hivyo ni makubwa na yanajitokeza baadae kulingana na matumizi yake

No comments

Powered by Blogger.