HAYA NDIO MAMBO KUMI(10) YANAYOYATAFUTWA SANA NA WATANZANIA KWENYE MTANDAO


Maendeleo ya sayansi na Teknolojia yameleta neema na mapinduzi makubwa Duniani. Tofauti na nchi zilizoendelea ambazo zimeingia kwenye ulimwengu wa mtandao muda mrefu, Suala la mtandao linaonekana Jipya kwa watanzania walio wengi, na Wengi wao wanatamanI kuona kuna nini huko ndani? Ujio wa simu za kisasa (smartphones) umekuwa jibu na suluhisho la tatizo hilo. Hivi ni Vitu Kumi Zaidi Wanavyovitafuta Watanzania (Kwa mujibu wa Kitafutio cha Google)

10.Biashara
Kutokana na kukua kwa kasi kwa uuzaji na ununuzi pepe (e-commerce) duniani, watanzania hawajaachwa nyuma sana japo ni idadi ndogo sana ya watanzania wanaoweza kufanya biashara mtandaoni. Wengi wa watanzania hutafuta na kuuza Magari, Simu za mkononi, pikipiki, nyumba na maeneo ya ardhi.



9.Vichekesho (comedy)
Utashangaa lakini hii ni moja ya vitu ya vitu vinavyotafutwa sana na Watanzania wengi kwenye mtandao, Wengi hutafuta video za kuchekesha, picha, na meseji za vichekesho. pia hupenda kuwajua wachekeshaji nk.


8.Elimu, mafunzo na afya
Kwa kiasi fulani kuna idadi ya watu wanaoingia kwenye mtandao kupata elimu inaongezeka, japo wahusika wengi hapa huwa wanafunzi hasa wa vyuoni ambao wengi hutumia google kupata majibu ya maswali waliyopewa na wakufunzi wao!


ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI



7.Michezo
Utakubaliana na mimi  kwamba watanzania wengi ni wapenda michezo (JAPO HAWAPENDI MAZOEZI YA VIUNGO) Wengi wa Watanzania huingia mtandaoni kupata habari za soka hasa za bara la ulaya.


6.Siasa
Uelewa wa Watanzania katika Siasa umekua ukiongezeka siku hadi siku na kumekuwa na idadi kubwa sana ya Watanzania wanaotafuta habari za siasa mfano; bunge, bajeti ya nchi, mahusiano ya nchi yetu na mataifa mengine, Vyama vya siasa nk.


5. Mahusiano & Kutafuta wapenzi
Kama ilivyo kwa nchi nyingi Duniani, Kumekuwa na idadi kubwa sana ya watu wanaotembelea mitandao ya kutafuta wapenzi, ushauri wa mapenzi, nk japo kuna unafuu kwetu (pengine ni kutokana na kutokuwa na uwezo wa kupata intaneti) kulingananisha ni nchi zingine kama nigeria na kenya.


4. Kutafuta Video, Muziki , na Programu za computer/simu
Kuna idadi kubwa sana ya Watanzania Wanaotafuta vitu hivi, Cha ajabu na Kwamba Video nyingi zinazotafutwa ni zile zenye maudhui ya kikubwa (adult movies). Pia nyimbo Zinazoangaliwa zaidi youtube ni zile zinazoonesha watu wakicheza bila maadili.


3. Kusoma na Kutuma Barua pepe
Watanzania walio na uwezo wa kuingia mtandaoni, Wengi wao wana anuani za Barua pepe japo ukweli ni kwamba kati ya watanzania 10 wenye anuani za barua pepe, ni watanzania watatu (3) tu ndio wenye Uelewa juu ya barua pepe na kuzitumia. 7 waliobaki pengine walifungua anuani ya barua pepe kwa kushurutishwa au ili tu wajiunge na mtandao fulan wa kijamii hasa facebook.


2.Blog na Magazeti
Blog na Magazeti zinashika nafasi ya pili kati ya vitu vinavyosomwa zaidi na watanzania kwenye Mtandao. Watanzania wengi hupenda kujua habari muhimu kuhusu yanayoendelea nyumbani na kimataifa pia, michezo, burudan nk. Watanzania pia hupenda kuangalia watu fulani mashuhuri kupitia blogs mbalimbali.


1. Mitandao ya kijamii
Najua utakubaliana na mimi kwamba karibu kila mwenye uwezo wa kuingia mtandaoni basi ameshajiunga na moja kati ya mitandao ya kijamii kama facebook, twitter, LinkedIn, Instagram, nk. Hii ndio inayoongoza kutembelewa na watanzania walio wengi zaidi kuliko kingine chochote.


MAKALA HII NI KWA HISANI YA KUMI MUHIMU

No comments

Powered by Blogger.