JESHI LA POLISI MKOANI MTWARA LIMEFANIKIWA KUDHIBITI MAANDAMANO YA CHADEMA.

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Jeshi la polisi mkoani Mtwara limefanikiwa kudhibiti maandamano ya chama cha maendeleo na demokrasia Chadema kwa kufanya doria kila kona ya mji huo huku wakiwa wamejiandaa kwa vifaa ili kupambana na yeyote atakayejaribu kuvunja katazo la jeshi hilo la kuzuia maandamano mkoani humo.
Hata hivyo ITV imeshuhudia jeshi hilo likiwa katika gari la polisi likipita maeneo mbalimbali likiwemo eneo la Mkanaledi ambalo lilitajwa maandamao ya Chadema yataanzia huko na hatimaye kuingia katikati ya mji.
Akizungumzia ulinzi huo kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara Augustino Ulomi amesema wamelazimika kutawanya askari kila kona sambamba  na kuwaita viongozi wa chama hicho kuwahoji baada ya kugoma kutii amri ya jeshi hilo ya kuzuia maandamano na kuamua kusambaza vipeperushi vya kushawishi wananchi kujitokeza katika maandamano kupinga kuendelea kwa bunge maalum la katiba
Kwa upande wake mwenyekiti wa chadema wilaya ya Mtwara Ibrahimu mandoa amesema pamoja na jeshi la polisi kufanikiwa kudhibiti maandamano hayo zipo njia mbadala za kufikisha ujumbe kwa umma na serikali.
Kwa upande wa wananchi wameonekana kutounga mkono maandamano hayo kwa madai waadhirika wakubwa ni wao.

CHANZO: ITV TANZANIA

No comments

Powered by Blogger.