ANASWA AKIJARIBU KUMTEKA MTOTO WA SHULE JIJINI DAR ACHEZEA KICHAPO CHA MBWA MWIZI
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Baadhi ya raia wenye hasira kali waliotoa kipigo ‘hevi’ kwa Bw. Omar wakiwa wametanda eneo la tukio. Akizungumza na Uwazi lililofika eneo la tukio ndani ya ‘dakika sifuri’, denti huyo aitwaye Laila alisema licha ya kuitikia salamu ya jibaba huyo na kumuamkia bado aliendelea kumchombeza na kila alipojaribu kumkwepa ilishindikana.
HALI bado tete! Polisi wa Kituo cha Magomeni jijini Dar,
wamemkamata baba mmoja aliyetambuliwa kwa jina moja la Omar baada ya kupokea
kipigo ‘hevi’ kutoka kwa raia wenye hasira kali akihusishwa na utekaji wa denti
wa Shule ya Msingi Mwalimu Nyerere iliyopo maeneo hayo.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Denti wa Shule ya Msingi Mwalimu Nyerere, Magomeni (mwenye
sare za shule) aliyenusurika kutekwa na njemba inayotambuliwa kwa jina moja la
Omar.
Tukio hilo lililokusanya kadamnasi lilijiri wikiendi
iliyopita, Magomeni-Kagera, Dar wakati mwanafunzi huyo akitokea shuleni.Kwa
mujibu wa mashuhuda, denti huyo alipofika eneo hilo, baba huyo alimsalimia na
baada ya kujibiwa salamu yake alianza kumchombeza kwa maneno matamu-tamu.
Makamanda wa Polisi waliofika eneo la tukio kumuokoa
mtuhumiwa.
Njemba huyo alivuka mipaka na kumshika mkono na kutaka
kumvutia ndani ya gari lililokuwa karibu yake ndipo Laila alipoamua kupiga
mayowe ya kuomba msaada na hatimaye kuokolewa na wasamaria wema waliokuwa
wakipita njia.
Mtuhumiwa (Omar) akiwa ndani ya gari mara baada ya kipigo.
Mwanafunzi huyo aliendelea kusema: “Alianza kunifuatilia
tangu kule, akanisalimia hujambo nikamjibu sijambo, akaniambia tena kwenu
hawajambo, nikamjibu hawajambo, akaendelea kuniambia eti, nimfuate akanipe
lambalamba, mimi nikakataa kwa sababu mama alinikataza kukubali kupewa lifti na
vitu vingine kutoka kwa watu nisiowajua tangu aliposikia habari za watoto
kutekwa na Noah nyeusi.
Wasamaria wema wakimuokoa mtoto huyo.
“Kila kitu nilimkatalia lakini yeye akawa anaendelea
kuniambia maneno yake na kuanza kunivuta ndipo nikaona sasa naenda kufa hivyo
ikanibidi nipige kelele ndiyo watu wakatokea na kumkamata kisha kuanza kumpiga
mpaka walipofika polisi.”
Mmoja wa wasamaria wema akimuingiza binti huyo kwenye gari
kumuondoa eneo la tukio.
Gazeti hili lilizungumza na mtuhumiwa aliyekuwa amehifadhiwa
ndani ya gari, alipoulizwa kuhusiana na tuhuma hizo alimuomba paparazi wetu
kabla ya yote kwanza amuokoe na kifo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali.
Binti akiwa kwenye gari mara baada ya kuokolewa.
“Chondechonde ndugu yangu, naomba kwanza mnilindie usalama
wangu, hao jamaa wanataka kuniua bila sababu, mimi wala sikuwa na nia mbaya na
huyo binti wananizushia tu, nilikuwa namsalimia tu,” alisema Omar kupitia
upenyo mdogo wa juu ya dirisha la gari alilohifadhiwa.CHANZO GPL
Post a Comment