CHID BENZ APATA DHAMANA BAADA YA KULALA GEREZANI SIKU MOJA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu. 



Na Mwene Said 
Hatimaye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemwachia kwa dhamana Msanii  wa Muziki wa Kizazi Kipya (bongo fleva), Rashidi  Makwaro (29), maarufa kama Chid Benz, baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya mahakaman hiyo.

Chid Benz, alifikishwa mahakamani hapo jana akikabiliwa na mashitaka matatu ikiwemo kukutwa na Dawa za kulevya aina ya Heroin yenye thamani ya Sh. 38,638, bangi ya Sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae.

Hakimu Mkazi Mkuu, Warialwande Lema alisema mshtakiwa alitakiwa kuwa na wadhamini wa wawili wanaotoka kwenye taasisi zinazotambulika na wasio walimu pamoja na kusaini hati ya dhamana ya Sh. milioni moja.

Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono akisaidiana na Inspekta Jackson Chidunda.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Wakili Kombakono alidai kuwa Oktoba 24, mwaka huu katika uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, uliopo Ilala jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alikutwa dawa za kulevya aina ya heroin isivyo halali zenye uzito wa gramu 0.85.

Katika shitaka la pili, ilidaiwa kuwa siku na eneo la tukio la kwanza, mshtakiwa alikutwa na gramu 1.72 za bangi isivyo halali.

Wakili huyo wa serikali alidai kuwa, siku na eneo la tukio la kwanza na la pili, mshtakiwa alikutwa akiwa na vifaa vinavyotumika kuvutia dawa za kulevya aina ya heroin, kigae na kijiko huku akijua ni kosa.

Mshtakiwa alikana mashitaka yote na upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Hakimu Lema alisema kesi hiyo itatajwa Novemba 11, mwaka huu.

No comments

Powered by Blogger.