HAYA NDIO MAMBO YA KUFANYA KAMA HUNA UJUZI UNAOHITAJIKA NA MWAJIRI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

Kitu cha msingi unapotafuta kazi inakubidi ufanye uchunguzi wa soko la ajira. Fuatilia nafasi za kazi zinazotangazwa ambazo zinakulenga wewe na utazame mambo yafuatayo;

Je ni nafasi gani imetangazwa?
Na naneno gani au Msamiati gani inatumiwa na mwajiri?
Angalia mshahara ni wa kiwango gani?
Na vigezo gani vinatumika kumpata huyo mtu?

Lakini je ufanyeje kama kazi iliyotangazwa inakuhusu, mshahara unahitaji, elimu unayo na vigezo vingine umekamilika, tatizo ujuzi anaohitaji mwajiri huna?
Kuna watu nimewaacha hapo, Je! ni wangapi wanajua kwamba watu wengi wana vyeti vizuri lakini wakipelekwa kazini wanachemka? Hapo ndipo ninapopaangalia zaidi kuliko shahada yako, stashada na vyeti kibao ulivyonavyo. Je una ujuzi gani unaobeba vyeti hivyo?

Inabidi ujifanyie utafiti mwenyewe na kujichunguza kama una nyenzo au ujuzi ambao utakufanya ukae kazini. Inawezekana vyeti vyako vizuri na CV yako imeshiba lakini ukiingia kazini mambo yanaanza kuwa magumu, ufanyeje?
Kabla ya kupata kazi inakubidi utumie mbinu kadha wa kadha kupata ujuzi, usibweteke, ushindani ni mkubwa hivyo jaribu kufanya mambo yafuatayo;

ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


Fanya kazi za kujitolea kujijengea Ujuzi
Jisomee sana kwa ile taaluma inayokuhusu
Fanya mazoezi ya Vitendo kwa taaluma unayosomea (Namaanisha usidanganye chuo ili uonekane ulifanya mazoezi ya vitendo ili kupata cheti.)
Kama kazi yako inahitaji sana mpaka uwe umeajiriwa ndipo upate ujuzi, basi soma sana kila kitu kinachohitajika kupata ujuzi na namna gani utaweza kuingia na kufanya kazi huko.
Hivyo uwe na moyo wa kujifunza na utayari wa kukuza ujuzi wako. Kama huna ujuzi wa kitu fulani jitahidi kukifanyia kazi. Mfano, nafasi ya kazi inahitaji mtu mwenye kujua namna ya kuwasiliana vizuri, ” Good communication skills” inamaanisha je una ujuzi wa kuwasiliana vizuri na watu au wateja au wafanyakazi wenzako?
Kitengo hicho kinahitaji mtu anayejua kuhusiana vizuri na watu wengine, kujua maneno ya kuongea, wapi kwa kuyaongea na wakati gani uyaongee. Je ni namna gani unaweza kuhusiana na watu wengine, Je wewe ni mtu ambaye unaweza kujenga na kuwa na marafiki? Je lugha yako ikoje? na vitu vingi sana vinavyohusisha ujuzi wa kuwasiliana n.k
Mwisho, unatakiwa kujua kazi inahitaji zaidi ya cheti ulichonacho. Je wewe una tofauti gani na watu wengine? Hapa tunaangalia ni namna gani unajikuza kitaaluma zaidi wewe mwenyewe kama utatafuta kazi au utatafutiwa kazi.

No comments

Powered by Blogger.