KAMPUNI YA KARIATI MATREKTA YAKABIDHI MATREKTA MANNE KWA WAKULIMA WA KONDOA NA MBARALI MKOANI MBEYA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu. 


 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kariati Matrekta, Alhaji Omari Kariati akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), wakati wa hafla ya kukabidhi matrekta hayo jijini Dar es Salaam leo. 
 Mmoja wa wakulima, Khalifa Huruvi  kutoka Kijiji cha Kwadelo Kondoa mkoani Dodoma akitoa maelezo yake baada ya kukabidhiwa trekta.
 Mkulima Sengeri Bakari naye akitoa maelezo yake baada ya kukabidhiwa trekta lake.
 Matrekta waliyokabidhiwa yanavyoonekana baada ya kuunganishwa.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kariati Matrekta, Alhaji Omari Kariati (kushoto), akifurahi wakati akijaribu moja ya matrekta hayo kabla ya kuwakabidhi wakulima hao. Kulia  ni mkulima Karoli Lubuva.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kariati Matrekta, Alhaji Omari Kariati (kushoto), akikata utepe kuashiria makabidhiano hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kariati Matrekta, Alhaji Omari Kariati, akimkabidhi funguo wa trekta, Mkulima Karoli Lubuva katika hafla hiyo. Wengine wanaoshuhudia tukio hilo ni wakulima kutoka Kwadelo mkoani Dodoma.

Na Mwandishi wetu


KAMPUNI ya Kariati Trekta imewakabidhi matrekta manne yenye thamani ya sh.milioni 100 kwa wakulima kutoka mkoani Mbeya na wilayani Kondoa baada ya kuwakopesha kwa bei nafuu.


Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kukabidhi matrekta hayo jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kariati Matrekta, Alhaji Omari Kariati alisema matrekta hayo yatawasaidia katika kilimo ambacho kitawainua kiuchumi.


Alisema kampuni hiyo kwa kipindi cha miaka miwili imewakopesha wakulima zaidi ya matrekta 84 ambapo kila anayekopa anatakiwa sh.milioni 25 kwa awamu mbili.


"Kila mkulima anaye kopeshwa kwa awamu ya kwanza anatakiwa kutoa sh.milioni 18 na baadae anamalizia kiasi kilichobaki" alisema Kariati.


Alisema kampuni yake hiyo imelenga kuwasaidia wakulima kuepukana na jembe la mkono na linatoa mkopo huo kwa mkulima yeyote ndani ya Tanzania.


Kariati alitoa mwito kwa wakulima kutumia fursa hiyo ya kukopa matrektra hayo ili kujikomboa kiuchumi na kustawisha maisha yao na kuondokana na umaskini.(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)

No comments

Powered by Blogger.