MH. MBOWE ATOA UFAFANUZI KUHUSU SUALA LA PICHA ZAKE AKIWA NA MKE WAKE KUSAMBAA MITANDAONI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu. 

Mbowe Ameongea haya Kuhusu hizo kwa kusema "Kwanza mke wangu alikuwa anatimiza umri wa miaka 50 ya kuzaliwa, vilevile firstborn wetu Dudley alikuwa amemaliza shahada yake ya kwanza Chuo Kikuu cha Sussex, Uingereza, kwa mambo hayo mawili, tuliona ipo haja ya kufanya sherehe, ukizingatia watoto wetu wengine wawili Nicole na Denis walikuwa wamerejea nchini kwa sababu nao wanasoma nje ya nchi." 

Siku hiyo ya tukio ilikuwa Jumapili, tulianza kwa kwenda kanisani Azania Front tukatoa sadaka, baada ya hapo tulikwenda Serena Hotel kwenye Ukumbi wa Kivukoni ambako chakula cha mchana kilikuwa kimeandaliwa, tukajumuika na ndugu wengine pamoja na marafiki.

Haikuwa sherehe tu kusema labda nilikurupuka kumbusu mke wangu, ilikuwa sherehe ya kifamilia, kumpongeza mke wangu na mtoto wetu, alisema Mbowe.

No comments

Powered by Blogger.