MOI YAJIIMARISHA KATIKA UTOAJI HUDUMA MUHIMU ZA TIBA NA UPASUAJI
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Afisa
Uhusiano wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu
(MOI) Bw. Patrick Mvungi akieleza kwa vyombo vya habari(hawapo pichani) kuhusu
mafanikio ya Taasisi hiyo ikiwemo kufanikiwa kwa zaidi ya asilimia 95 ya kutoa
huduma muhimu za Tiba na Upasuaji kwa wagonjwa wanaopokelewa na hivyo kupunguza
vifo na rufaa za kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi,wakati wa mkutano uliofanyika
leo Jijini Dar ea Salaam. Kushoto ni Meneja Ustawi wa Jamii na Uhusiano wa
Taasisi hiyo Bw. Almas Jumaa.
Meneja
Ustawi wa Jamii na Uhusiano wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na
Mishipa ya Fahamu (MOI) Bw. Almas Jumaa akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo
pichani) jinsi Taasisi hiyo ilivyoendelea kuwa nguzo Muhimu katika kuokoa
maisha ya watanzania ambapo upasuaji wa kitaalam wa mgongo umeendelea kufanyika
na kufanikiwa kwa zaidi ya asilimia 99 na kusaidia kuwaondoa wagonjwa wenye
tatizo hilo katika hatari ya kupotea uhai.Kulia ni Afisa Uhusiano wa Taasisi
hiyo Bw. Patrick Mvungi.PICHA
NA MAELEZO.
Na
Hassan Silayo-MAELEZO
Taasisi
ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) imeendelea
kuwa nguzo muhimu nchini katika utoaji wa huduma za tiba na upasuaji. Hayo
yamesemwa na Afisa Uhusiano wa Taasisi hiyo Bw. Patrick Mvungi wakati wa
Mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.
Patrick
amesema kuwa MOI imesaidia kuokoa zaidi ya asilimia 95 ya watanzania ambao kwa
namna moja au nyingine wangeweza kupoteza maisha yao au kupata ulemavu wa kudumu kutokana na ajali.
“MOI
kwa kiasi kikubwa imefanikiwa kuokoa maisha ya watanzania kwa zaidi ya asilimia
95 kutokana na kutoa huduma muhimu ya za tiba na upasuaji wa wagonjwa
wanaopokelewa na hivyo kupunguza vifo na rufaa za kuwapeleka wagonjwa nje ya
nchi” alisema Mvungi.
Akizungumzia
kuhusu upasuaji wa kitaalam wa mgongo (specialized Spine Surgeries) Mvungi
alisema kuwa Taasisi hiyo imeendelea kufanya na zaidi ya asilimia 99 ya
wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wamepona na kurudi katika hali zao za kawaida. Naye
Meneja Ustawi wa Jamii na Uhusiano wa Taasisi Taasisi hiyo Bw. Almas Jumaa
alisema kuwa zaidi ya wagonjwa 1,256 ya wagonjwa wa upasuaji mkubwa wa nyonga
walipasuliwa salama na zaidi ya asilimia 95 ya wagonjwa hao wamepona kabisa.
Pia
Almas alisema kuwa pia Taasisi imeendelea kutoa matibabu ya magonjwa ya ubongo
yaliyokuwa yanahitaji upasuaji yamefanikiwa kufanyika kwa zaidi ya asilimia 80
na wagonjwa waliokuwa na matatizo hayo wamepona na kuondolewa kwenye hatari ya
kupoteza uhai.
Taasisi
ya MOI imewataka watanzania kuitumia Taasisi hiyo na kuacha kufuata matibabu
nje ya nchi kwa gharama kubwa tofauti na kama wangepata huduma hizo hapa nchini
kwa gharama nafuu.
Post a Comment