MTAZAMO WA MDAU ALEX THOMAS KUHUSIANA NA MISS TZ 2014: SAKATA LA MISS TANZANIA NI MUENDELEZO WA UFISADI.

 Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu. 


Miss Tz 2014 Sitti Abbas Mtemvu

Na. Alex Nicholaus Thomas. Dodoma.

Sikuwa napenda na mimi siku moja kujadili masuala ya umiss kwa sababu kwangu ni masuala yenye mchango mdogo sana katika ustawi wa watanzania wengi ambao ni masikini.

Lakini leo nimelazimika kuzungumzia au kusema neno dhidi ya mshindi wa Redd's Miss Tanzania 2014, Sitti Z. Mtevu kwa mtizamo wa matokeo ya misingi mibovu kama Rushwa, Ufisadi, Ujanja Ujanja kwenye Uongozi wa Nchi yetu.

Wahenga wanasema usipoziba ufa utajenga ukuta. Upendeleo, kubebana, Ubinafsi ambao umeendelea kumea na kupaliliwa na mifumo yetu ya uendeshaji wa nchi, umetufikisha hapa tulipo kama taifa masikini sana duniani, taifa lisilo na Dira wala muelekeo.

Ni vyema tujue kila baya linalotukabili sasa halijatokea kwa bahati mbaya, bali ni matokeo ya kupuuzia kusimamia kwa ukamilifu baadhi ya mambo ya msingi. Unalalamikaje kuna Umasikini wakati wewe ndiye unaeuleta kwa kuweka watumishi wa umma wasio na sifa ila tu ni kwa sababu wanafahamiana na watawala.

Mathani, tumekuwa tukishuhudia uongozi wa nchi na kazi katika maeneo nyeti kama BOT, wizarani, na kwenye Taasisi nyeti za serikali zikishikiliwa na watoto wa wazito(vigogo) lakini watawala waliopewa dhamana ya kuyakemea hayo ndio kwanza wameziba macho na masikio, lakini kwa mlango wa nyuma hao hao wanajidai kukemea Ukabila na Udini bila kujua wao ndio wanaoupalilia udini na ukabila huo. Kujuana kukiwa ndio msingi wa mtu kuajiriwa au kupata madaraka ni rahisi kuchokonoa hisia za udini na ukabila.

Kudhihirisha tabia hii ya kujuana na kubebana kwenye mambo mbali mbali nchini inakuwa na kumea kwa kasi kubwa, sasa hivi hadi kwenye mambo ya urembo na ulimbwende ili ushinde ni lazima uwe mtoto wa mkubwa au kiongozi hata kama huna sifa ya kufuzu nafasi hiyo alimradi ni mtoto wa mkubwa basi umeshinda.

Ndio yaliotokea kwenye mashindano ya Redd's Miss Tanzania 2014, kama matokeo ya kushamiri kwa udugu na kubebana (Nepotism). Madamu Sitti Mtemvu (Miss Tanzania 2014) ni mtoto wa kigogo basi ameshinda taji hilo japo hana sifa kabisa.

Mkimfuatilia unaona ni mtu alieshinda kwenye hali za mizengwe sana mfano ukifuatilia mahojiano yake na waandishi wa habari anajikanyaga na kushindwa kuthibisha umri wake kamili. Utasikia mara ana miaka 18, alipobanwa sana akadai ana miaka 23, lakini passpot yake na Driving Lessen yake inaonesha ana miaka 25 na bado wanaomjua wana sema ana mtoto wa miaka 4 na wametoa hadi picha ya mtoto wake ambavyo vyote hivyo ameshindwa kuvikana mbele ya waandishi wa habari.

Kweli kama angekuwa anaandamwa na vyombo vya habari bila sababu kama anavyojitetea, hakuwa na haja ya kujiuma uma kwenye kuelezea swali la kama anamtoto au la, na swali la kama passport na driving lessen yake vilivyopo kwenye mitandao ni vyake halisi au laa. Nilitegemea angetumia fursa hiyo ya kuzungumza na waandishi wa habari kujibu utata huo kwa kujiamini lakini ni ujanja ujanj tu.

Hivi tumekosa watanzania warembo na wenye vigezo vya kushinda Redds Miss Tanzania 2014 mpaka tunakuja chagua kibibi kizee kama Sitti Mtemvu? Alikuwa wapi wakati huo alipokuwa binti asigombee mpaka sasa hivi kazeeka anakuja kung'ang'ania mambo ya mabinti?

Rai yangu kwa Basata na Mdhamini mkuu wa miss Tanzania 2014 wafanye uchunguzi na kumvua taji hili Sitti Z. Mtemvu na kumfikisha mahakamani kwa kughushi nyaraka za serikali kama cheti feki cha kuzaliwa alichonesha waandishi wa habari. Kama Basata na Redds watashindwa kufanya hivyo ni wazi tutakosa imani nao. Na nashauri watu wasusie bidhaa huduma zao.
Pia natoa wito kwa wadau wa Urembo Tanzania kuwaandikia shirikisho la "Miss" duniani kuwasilisha malalamiko haya ili ikiwezekana Miss Tanzania ifungiwe ili kutoa funzo na kukomesha tabia hii mbaya ya kubebana.
Na Viongozi wa kamati ya Miss Tanzania

Ni lazima wajue kuwa kufanya kwao vibaya kila mara kwenye mashindano ya dunia ya walimbwende ni kwa sababu ya kuchagua mshindi anaewakilisha taifa kwa minajiri ya kujuana bila kuzingatia sifa mahsusi. Watashika mkia kila mara kama hawatajirekebisha.


Ukiona kunafuka moshi ujue kuna moto haya ni matokeo ya mifumo mibovu inayoendekezwa na serikali yetu na huu ni mwanzo makubwa yanakuja na hayo tuombee Mungu ayaepushe na machafuko.

No comments

Powered by Blogger.