PICHA: YALIYOJIRI KWENYE MKUTANO WA BAWACHA MJINI BUKOBA MKOANI KAGERA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

Mwenyekiti Bawacha Mhe. Halima Mdee akizungumza na wananchi waliofika kwenye mkutano huo uliofanyika jana jioni Katika Uwanja wa Uhuru, Mjini Bukoba mkoani Kagera.

Baadhi ya wanachama wapya wa Chadema wakiongea na wananchi kuhusu sababu iliyomfanya kurejesha kadi ya CCM na Kujiunga na Chadema.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
 Katikati ni Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare
Mbunge wa Viti Maalumu ambaye pia ni katibu wa mkoa, Mama Concesta Rwamlaza akiongea na maelfu ya wananchi waliojitokeza katika Mkutano wa BAWACHA jana Mjini Bukoba

Mwenyekiti Bawacha Mhe. Halima Mdee akikabidhiwa zawadi kutoka kwa Wanawake wa Chadema Kata ya Hamugembe Mjini Bukoba.
Sehemu ya wanachi wa Manispaa ya Mji Bukoba waliojitokeza katika Mkutano wa hadhara wa Viongozi wa BAWACHA uliofanyika jana jioni ya Oktoba 29 Katika Uwanja wa Uhuru Mjini Bukoba mkoani Kagera.
Mwenyekiti Bawacha Mhe. Halima Mdee akiondoka kwenye mkutano huo

 Agenda kuu katika mkutano huo ni:
 i) Kuwahamasiha wanawake kujiandikisha katika daftari la kudumu la kupiga kura
(BVR)
ii) Kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa
iii) Kuwaelimisha na kuwa na mtazamo sahihi wa katiba mpya ijayo
iv) Kuwahamasisha kushiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015
v) Kubaini na kuwatia shime wagombea wanawake makini katika nafasi mbalimbali
kwenye chaguzi hizi


PICHA ZOTE NI KWA HISANI YA BUKOBA WADAU BLOG

No comments

Powered by Blogger.