TBC 1 YASHIKA NAFASI YA MWISHO.
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Kwa hali ya
kushangaza, kituo cha television cha matangazo cha tbc 1 kati ya vituo
vinne maarufu vya matangazo ya habari nchini Tanzania kimeshika nafasi
ya mwisho baada ya kufanyiwa utafiti,
Kwa habari za uhakika
ni kwamba kituo kilichoongoza kuangaliwa na watazamaji wengi ni ITV
kikifuatiwa na Star TV, nafasi ya tatu imeshikwa na Channel 10 na
hatimaye TBC1.
Kwa utafiti uliofanya
na na TCRA imebainika kuwa ni aibu kama kituo television ambacho ni cha
Taifa na ni UMMA kushika mkia nyuma ya vituo binafsi jambo ambalo ni
hatari.
Vyanzo vya kuaminika
vinadai kuwa TBC1 imefikia hapi baada ya kugundulika inabagua baadhi ya
habari ya vyama vya siasa na kutoa habari ya chama kimoja tuu jambo
ambalo siyo sahihi katika utashi wa utangazaji na kutofuata uhuru wa
kiutangazaji ndani ya uongozi wa shirika la habari la Tanzania,
Utafiti umeonyesha
kuwa ili chombo cha habri kiweze kuangaliwa na watu wote wa vyama vyote
ni lazima chombo cha habari kitoe habari bila kubagua vyama vya siasa
maana watazamaji wana misimamo tofauti na itikadi tofauti, na kama
chombo cha habari kikiamua kutoa habari kwa chama kimoja cha siasa basi
ujue hapo watakaoangali hizo taarifa za habari ni hao hao wa chama
kimoja.
Watafiti pia walienda
mbali zaidi na kukinyoshea vidole kituo cha taifa cha utangazaji kuwa
ni chombo cha UMMA na kisipende kubagua baadhi ya taarifa za habari za
vyama vya siasa kwa misingi ya kuelekezwa na wanasiasa au viongozi wa
nchi maana madhara yake ni wananchi kushindwa kuangalia hicho kituo.
Mwisho wake
kitashindwa kufanya biashara na hatimaye kutegemea tuu ruzuku serikalini
na hapo ndo nchi itazidi kupata hasara badala ya kukiacha chombo
kijiendeshe kwa uhuru. Wametoa mfano kama shirika la habari la Uingereza
BBC lingefanya kama TBC inavyofanya basi nayo ingeishia kutazamwa tuu
nchini uingereza na tena kwa watu wachache tofauti na ilivyo sasa BBC
inatazamwa duniani kote.
Utafiti umeonyesha
kuwa hivi vyombo vingine vya habari ITV, Star TV na Channel 10 vimepata
watazamaji wengi kwa kuwa havibagui matangazo ya kada tofauti ya vyama
vya siasa na hapo ndoo inasababisha waweze kupata watazamaji wa
kutosha.
chanzo Lukaza Blog
Post a Comment