UPDATES: NAIBU WAZIRI ARUSHIANA RISASI NA MWANAYE MKOANI MOROGORO

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu. 

Zimezagaa taarifa kuwa Naibu Waziri wa zamani wa Afya na mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Lucy Nkya (PICHANI), amerushiana risasi za moto na mwanaye wa kumzaa, Jonas Nkya ndani ya ofisi zao mkoani Morogoro muda huu.

Lakini Kwa mujibu wa mtoto wa waziri huyo John Nkya ambaye amezungumza na mwandishi wa habari Hilda Mushi amekana kurushiana risasi na mama yake mzazi na kusema hakuna kitu kama hicho

Amesema ukweli ni kwamba alikuwa amekwenda kwenye eneo la ofisi yao kwa ajili ya kwenda kuchukua gari ili aende shamba na ghafla silaha aliyokuwa nayo ilidondoka na kufyatua risasi moja jambo lililozua taharuki kwa watu



"Mimi sina ugomvi wowote na mama na hizi taarifa ni za uongo, ukweli ni huo nilioueleza ndugu mwandishi, kwanza mama yangu mwenyewe hana silaha sasa nashangaa imekuwaje tukagombana na kufyatuliana risasi, kama ingekuwa adhma yangu ningelifanya tukio hili nyumbani sasa iweje ofisini? alisema John

"Kwanza mimi nashangaa hizi taarifa maana nilikuwa shambani baada ya kurudi nashangaa nakutana na waandishi wa habari wananihoju kujua kuhusu tukio hilo, na tayari pia taarifa zimeshazagaa kwenye mitandao ya kijamii, ndugu mwandishi huo ni uongo sijafyatuliana risasi na mama yangu" amesema


Taarifa zaidi zitakujia endelea kusoma eddy blog

No comments

Powered by Blogger.