YP AZIKWA MAKABURI YA CHANG'OMBE JIJINI DAR ES SALAAM

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

Marehemu Yesaya Ambikile Mwakalekamo 'YP' amezikwa jana katika makaburi ya Changombe jijini Dar es salaam.
Marehemu YP alifariki juzi baada ya kuugua kifua na kulazwa katika Hospitali ya Temeke hadi mauti yalipo mkuta.
Awali kabla ya maziko hayo YP aliagwa na ndugu jamaa na marafiki zake katika viwanja vya sigara Chang'ombe ambapo wasanii mbalimbali wa muziki wa Bongo fleva na Bongo muvi walihudhuria.
YP kabla ya kuhamia katika sanaa ya uimbaji na kuibuka na kundi la wanaume Family alikuwa akifanya sanaa ya maigizo na vichekesho akiwa kundi moja na wasanii, Masanja Mkandamizaji, Mpigapicha maarufu na Blogger Mroki Mroki, Kiwewe, Dokii enzi hizo wakiwa na kundi la Get Well Generation lililokuwa chini ya Dokii na kurusha michezo yake Star Tv.
YP enzi za uhai wake aklitamba na nyimbo kama 'Ulipenda Pesa', 'Pumzika', 'Shemsha' na nyimbo nyingi za TMK Wanaume Family kama 'Twende zetu' ya Chege, 'Dar mpaka Moro', 'Kichwa kinauma', 'Tufurahi' na nyimbo nyingi za TMK Wanaume family pia alivuma na wimbo wa Binadamu Visa alioimba na swahiba wake, Y-Dash.

ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Kiongozi wa kundi la Yamoto Band na TMK, Mkubwa na Wanawe, Saidi Fela akizungumza wakati wa msiba huo. 
Juma Nature kutoka TMK Wanaume Halisi akizungumza.
Mh Temba nae akizungumza...
Mmoja wa waigizaji aliyehudhuria mazishi hayo, Jacob Steven 'JB' akizungumza.
Ilikuwa ni vilio kutoka kwa kila mtu aliyehudhuria mazishi hayo. 
Picha kwa hisani ya Father Kidevu

No comments

Powered by Blogger.