AJALI YATOKEA MKOANI TANGA BAADA YA TOYOTA COASTER KUGONGANA NA SCANIA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

Baadhi ya watu wakishuhudia ajali ya basi aina ya Costal lenye namba za usajili T410 BJD lililokuwa likifanya safari zake kati ya Tanga na Lushoto likiwa limepinduka baada ya kugongana na Scania lenye namba namba T645 ABJ katika kijiji cha mkanyageni wilayani Muheza na kusababisha vifo vya watu 14. (Picha na Elizabeth Kilindi)
Mganga Mfawidhi wa hospitali ya teule wilayani Muheza, Rajabu Malamhiyo (kushoto) akiangalia hali ya majeruhi ambaye ni dereva wa Scania iliyopata ajali yenye namba za usajili T645 ABJ Benjamini Abeid.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


Watu 11 wamekufa na wengine 25 kujeruhi vibaya baada ya basi dogo aina ya Coaster la kampuni ya ''Thende Sheki'' kugongana uso kwa uso na lori la mizigo katika eneo la mkanyageni lililopo wilayani muheza.
Ajali hiyo ilikusanya mamia ya wananchi kutoka jijini tanga,muheza na lushoto kwa ajili ya kwenda kushuhudia na kutambua miili ya marehemu iliyokuwa imehifadhiwa nje katika hospitali teule ya mtakatifu augustino wilayani muheza kwa ajili ya utambuzi ambapo hadi majira ya mchana miili ya watu 9 waliokufa papo hapo katika eneo la tukio ilitambuliwa na ndugu na jamaa.
 
Akielezea miili na majeruhi waliopokelewa katika hospitali hiyo,kaimu mganga mkuu wa wilaya ya muheza Dkt.Perter Shemkhai amesema watu wawili walifariki hospitali muda mchache baada ya kuletwa na kupatiwa tiba katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).
 

Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo wamesema dereva mwenye lori alikuwa akiyumba njia nzima kabla ya kukutana uso kwa uso na gari dogo la abiria aina ya Coaster hatua waliyodai kuwa ina viashiria vya dereva wa lori hilo alikuwa amepitiwa na usingizi wakati akiwa barabarani. 

No comments

Powered by Blogger.