KONGAMANO LA 31 LA KISAYANSI LAENDELEA MJINI BAGAMOYO

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu. DSC_0825
Maximilian Mapunda kutoka shirika la Afya Duniani (WHO-Country Officer) akiwasilisha mada kwenye kongamano hilo.
Na Andrew Chale, Bagamoyo
Pichani ni baadhi ya picha za matukio ya siku ya pili, jana Novemba 25 kwenye kongamano la Kisayansi la 31, '31th Annual Scientific Conference and Annual General Meeting'.. lililoandaliwa na Tanzania Public Health Association (TPHA).
Mkutano huo unafanyika mjini hapa Bagamoyo katika Ukumbi wa Stella Maris, Bagamoyo, Pwani Tanzania.
Kongamano hilo la kisayansi la 31, limeanza Novemba 24 linatarajia kuwa la siku tano na kutarajia kumalizika Novemba 28 ambapo wataalamu wa afya na wadau watajadilina mambo mbalimbali ya afya hapa nchini.
DSC_0830
Katibu Mtendaji wa TPHA Taifa, Dk. Oberlin Kisanga akiwasilisha mada maalum kwenye kongamano hilo.

DSC_0852
Dk. Ali Mzige mshiriki wa Kongamano la Kisayansi la 31, akiwasilisha mada maalum.
DSC_0848
Mwenyekiti wa TPHA Taifa, Dk.Elihuruma Nangawe akitoa ufafanuzi kwenye mada zinazotolewa na wajumbe kwenye kongamano hilo.
DSC_0856
Wajumbe wa kongamano hilo wakichangia mada.
DSC_0857
Katibu Mtendaji wa TPHA Taifa, Dk. Oberlin Kisanga (kushoto) akifuatilia kwa makini kongamano hlo.

No comments

Powered by Blogger.