SEND OFF PARTY YA NOREEN MHINA YAFANA JIJINI DAR

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 
 Bibi Harusi Mtarajiwa Noreen Mhina  akiwa katika nyuso ya Furaha, jana tarehe 25.11.2014
  
 Bibi Harusi Mtarajiwa Noreen akiwa amempata Mume wake mtarajiwa Leonard  Baada ya kumsaka ukumbi Mzima kwa ajili ya kumtambulisha kwa wageni waalikwa .

 Bibi harusi Mtarajiwa Noreen akimvisha Mume wake mtarajiwa Leonard  zawadi ya Saa Mara baada ya kutambulishwa Rasmi wa wageni waliofika katika Sherehe ya kumuaga
Mc wa Sherehe hiyo ya Kumuaga Noreen Akiendelea na yake
 
 Bwana Harusi Mtarajiwa Leonard  akionesha zawadi yake ya saa aliyonunuliwa na Mke wake mtarajiwa Noreen ikiwa ni moja ya zawadi ya kufika kwake katika sherehe hiyo
 
 Mume Mtarajiwa Leonard  wa Noreen akiwa anamlisha  Chakula Mkewe Mtarajiwa ishara ya Upendo
Msemaji wa upande wa Bwana harusi mtarajiwa akiwakaribisha Rasmi katika harusi upande wa wazazi wa Noreen, Ndugu jamaa na marafiki na kutoa nasaha chache. Jana Tarehe 25.11.2014

Meza ya wazazi wa upande wa Bibi harusi mtarajiwa wakiwa wanasikiliza Nasaha kutoka kwa msemaji wa upande wa Bwana Harusi mtarajiwa.
Wadada wa Mujini nao walimwagia pesa za kutosha Noreen..
Baadhi ya Marafiki wakubwa wa Noreen aliosoma nao katika chuo cha CBE Dodoma
Palikuwa hapatoshi hapa ambapo Noreen na Bwana Harusi Mtarajiwa Leonard  pamoja na wageni wengine waalikwa walicheza kwaito ya nguvu..
Burudani ya Nguvu inaendelea hapa..
Kama kawaida wale mapaparazi wa kujitegemea hawakosi kupata ukodaki wa nguvu kwa ajili ya Facebook, Twitter, Instagram, Whatsapp na kwengine kwingi kuifanya sherehe kuwa inanoga zaidi
Baadhi ya Wageni waalikwa wakifuatilia Sherehe na kufurahi.
Bibi Harusi Mtarajiwa akiwa anapunga mikono kuaga wageni waalikwa ishara ya kuondoka ukumbini kwenda kupumzika na kujiandaa na harusi huku akisindikizwa na wapambe wa kutosha.

No comments

Powered by Blogger.