WATU WANNE WANAO SADIKIWA WEZI WA MIFUGO WAMEUWAWA KWA KUPIGWA NA KUCHOMWA MOTO WILAYANI IRAMBA.

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu. 

Watu wanne wanao sadikiwa kuwa wezi wa ng’ombe wameuawa na watu wenye hasira zaidi ya sabini , kwa kupigwa  na kuchomwa moto katika kijiji cha sheluhi wilayani iramba, baada ya kukutwa wakiwa wamewachinja ngo’mbe hao.
Akithibitisha kutokea kwa mauaji hayo  mwenye kiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya iramba ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo Bwana Yahaya Nawanda amewataka wananchi wanapo wakamata wahalifu kuacha vitendo vya kujichukulia hatua  za kuwauwa kwa kufanya hivyo wanakuwa hawalisaidii jeshi lapolisi.
 
kwaupande wake mama wa mmoja wa marehemu  pamoja na mashuhuda wamesema kitendo cha  mauaji yaliyo fanywa na  wananchi wenye hasira ,hawa kufanya jambo la busara kwani  wange pelekwa kwenye vyombo vya sheria.
 
Vitendo vya wananchi kuamua kuwauwa wahalifu katika wilaya ya iramba vimekuwa vikishamiri  jambo ambalo siyo sahihi  kwani  wamekuwa wakipoteza ushahidi na kupatikana kwa wahalifu wengine.

CHANZO: ITV TANZANIA

No comments

Powered by Blogger.