BREAKING NEWS: WAZIRI ANNA TIBAIJUKA AMEVULIWA RASMI UWAZIRI NA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AWEKWA KIPORO

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Anna Tibaijuka ametenguliwa rasmi nafasi yake ya Uwaziri na Rais Jakaya Kikwete
Rais Jakaya Kikwete amesema "Waziri wa ardhi, tumekaa nae na kuzungumza. Pesa hizi ni za nini na kwa ajili gani na amesema ni za shule, mengi yameelezwa. Maswali makubwa kwa nini hazijaenda shuleni moja kwa moja na zikawa kwa jina lake, akasema ndo masharti ya mtoaji, tumelitafakari sana na tumeona msingi mkubwa wa kimaadili kuhusu kupokea hizi pesa, tumeshazungumza nae na tumemwambia atupe nafasi tumteue mwingine.
Pia ameongezea kwa kusema kuwa"Waziri wa nishati na madini tumemuweka kiporo, kuna uchunguzi nimeagiza ufanywe na nikipata majibu nitafanya uamuzi, tume ya maadili pia wanafanya kwa ajili ya kupata maamuzi kwa misingi ya haki."

No comments

Powered by Blogger.