KOREA KASKAZINI YATISHIA KUISHAMBULIA IKULU YA MAREKANI KUFUATIA SHUTUMA ZA UDUKUZI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Kwa mujibu wa Korea Kaskazini, Rais Barack Obama amekurupuka kusambaza uongo kuwa nchi hiyo ilishiriki kufanya shambulio la mtandaoni ndani ya mifumo ya kampuni ya Sony Pictures.

Pia imeonya kuishambulia Ikulu ya Marekani, Pentagon na Marekani yote. Marekani inaishutumu Korea kuhusika kwenye udukuzi huo ulioifanya Sony isitishe kufanya uzinduzi wa filamu yake, The Interview inayoongelea kuuawa kwa kiongozi wake, Kim Jong-un. Jeshi la Korea Kusini limeonya kuwa lipo tayari kutumia njia zote za kivita dhidi ya Marekani.
Korea Kaskazini imesema inafahamu jinsi ya kuthibitisha kuwa haihusiki na udukuzi huo na imependekeza uchunguzi wa pamoja na Marekani. Nchi hizo ziliwahi kuingia vitani mwaka 1950-53 kwenye vita vya Korea.

CHANZO: BBC

No comments

Powered by Blogger.