UBOVU WA MELI YA MV VICTORIA WAZUA MAKUBWA, ABIRIA WAANDAMANA HADI KWA MKUU WA MKOA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu. 


Meli ya MV Victoria inayofanya safari zake kutoka mkoani Kagera kuelekea jijini mwanza  imezuiliwa kuondoka mjini bukoba kutokana ubovu ilionao hali ambayo imewalazimu wananchi waliokuwa wanataka kusafiri na meli hiyo kuandamana hadi kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kagera kwa ajili ya kutoa malalamiko yao.

Wakiongea   nnje ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kagera  John Mongela wananchi hao wamelalamikia kuto kuwepo kwa usafiri wa meli kwa zaidi ya mwezi moja  sasa na kwamba jana meli hiyo imewasili mjini Bukoba na kuambiwa wapakie mizigo yao ndani ya meli hiyo kwaajili ya kuisafirisha  kutoka mkoani kagera kueelekea jijini Mwanza ambapo wamesema wamepakia mizigo yao ndani ya meli hiyo na leo wameambiwa meli hiyo haitosafiri kutokana na meli hiyo kuwa na hitilafu tangu muda mrefu na kwamba mazao yao biashara sasa  yamekuwa yakiharibika ndani ya meli hiyo  hali Ambayo imewalazimu wananchi hao kuandamana mpaka kwenye ofisi za mkuu wa mkoa wa kagera kwaajili ya kutoa malalamiko yao  juu ya meli hiyo.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Akizungumza na wananchi hao mkuu wa wilaya ya Bukoba Bi.Sipora Pangani amewataka wananchi  hao kuwa na subira  na kuwataka waondoke katika ofisi hizo  huku akisema kuwa serikali italishughulikia suala hilo  huku mbunge wa viti maalum Conchesta Rwamulaza akiitaka serikali kuiondoa meli hiyo kwakuwa imekuwa  ikileta hofu kubwa kwa wananchi wa mkoa huo na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake  meneja wa SUMATRA mkoa wa Kagera Alex Katama amesema  meli hiyo ilisimamishwa  kufanya kazi tangu ilipo pata hitilafu kwa ajili ya matengenezo lakini juzi meli hiyo iliondoka jijini Mwanza hadi mjini Bukoba bila Ruhusa  kutoka kwenye mamlaka husika  na akaongeza kuwa meli hiyo sasa ni mbovu na haifai kutoa huduma yoyote mpaka itakapo fanyiwa marekebisho.

No comments

Powered by Blogger.