UPDATES: MATOKEO YA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.



MATOKEO: 
Mabomu yatumika: Jeshi la Polisi limeamua kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi mkoani Mwanza katika maeneo ya Pasians, Mji Mwema, Kirumba, Ibungiro na Kitangiri baada ya vurugu wakati wa kusubiri kutangazwa matokeo.

Kijiji cha Muungano Kata ya Chahwa mkoani Dodoma: CHADEMA 196, ADC 38
Mbozi; Mtaa wa Masaki: CHADEMA 99, CCM 44
Kigoma Mjini; Mtaa wa Gezaulole: CHADEMA 240, CCM 198
Ukonga; Mtaa wa Kivule Majohe: CHADEMA 231, CCM 77
Musoma Vijijini; Kijiji cha Muhoji: CHADEMA 197, CCM 464
Ubungo; Mtaa wa Msewe: CHADEMA 683, CCM 356
Kinondoni; Mwenge Nzasa: CHADEMA 344, CCM 318
Mwanga Mtaa wa Lwami: CHADEMA 55, CCM 35
Mererani: CHADEMA imeshinda mitaa 7 kati ya 8

ENDELEA KUTIZAMA MATOKEO HAYA KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Kitongoji cha Endulele: CHADEMA 170, CCM 130
Monduli; Kitongoji Kambi ya Mkaa: CHADEMA 27, CCM 13
Mwanga Mtaa wa Lwami: CHADEMA 55, CCM 35
Arumeru Magharibi, Kitongoji Endulele: CHADEMA 170, CCM 130
Ushirombo Mjini: CHADEMA inaongoza vitongoji 10, CCM inaongoza vitongoji 4
Moshi Manispaa, Kitongoji Longuo A: CHADEMA 206, CCM 66
Mbozi Mtaa wa Mbugani: CHADEMA 227, CCM 160
Wilaya ya Muleba mkoani Kagera: CHADEMA imeshinda viti vyote vya vijiji

Wilaya ya Kyela  Butiama- CHADEMA
Kyela kati -CHADEMA
Roma -CHADEMA
Mikoroshoni -CCM
Mbugani -CHADEMA
Nazareti -CHADEMA
Unyakyusa -CCM
Kapwil- CCM
Itunge mashariki -CCM
KEIFO -CCM
OROFEA -CHADEMA
SAMA B -CCM
Mikumi -CHADEMA
Mwaikambo -CHADEMA
Kilasil- CCM
Mkombozi -CHADEMA
Bondeni A-CCM
Bondeni B-CHADEMA
Itunge-Mundekesye CHADEMA


Matokeo ya Lindi - Ruangwa

Nanjaru - CUF
Nambilanje - CUF
Mkaranga - CUF
Mtondo - CUF
Mchichili - CUF
Nahanga - CUF
Namienje - CUF
Chikundi - CCM
Chibula - CUF
Muhulu - CUF
Mbekenyela - CCM
Naunambe - CUF
Matambarale - CUF
Namkatila - CUF
Chuyu - CUF
Namikulo - CUF


Kata ya Mji Mpya, Morogoro yenye mitaa 12, CCM imeshinda mitaa 9, CHADEMA wakishinda mtaa 1 huku mitaa miwili mpaka sasa bado vurugu zimetanda baada ya kura kudaiwa kuzidi huku watu kadhaa wakituhumiwa kupiga kura mara mbili.
Kagondo, Kata ya Muhutwe, Kagera: CHADEMA imeshinda mitaa 4 kati ya 5
Kufungwa Vituo: Katika maeneo mengi vituo vya upigaji kura tayari vimefungwa huku wananchi wakisubiri kwa hamu kujua matokeo.
Uchaguzi Migombani: Uchaguzi wa Serikali za Mitaa eneo la Migombani, Segerea jijini Dar umeingia dosari baada ya Afisa Mtendaji Kata ya Segerea kutangaza kusitisha uchaguzi huo kimyakimya bila sababu za msingi ambapo wananchi waliamua kumweka mtu kati mpaka akaruhusu uchaguzi huo kuendelea kwa maandishi. Akijitetea afisa huyo alidai kuwa ameagizwa na Mkurungenzi wa Uchaguzi wa Manispaa ya Ilala kufanya hivyo.
Mazimbu, Morogoro: Eneo la Mazimbu, Moro kimenuka mpaka wanajeshi wamelazimika kuingilia kati kutuliza ghasia wakati wa zoezi la upigaji kura.
Kawe, Dar: Uchaguzi wadaiwa kuingia dosari baada ya mgombea wa CCM kutoa amri ya vitabu kufungwa kabla ya muda ulipangwa.
Kigogo, Dar: Mgogoro umezuka katika Kituo cha uchaguzi Kigogo jijini Dar baada ya wananchi kudai kuwa baadhi ya watu wamepelekwa kama mamluki eneo hilo kwa ajili ya kugipa kura.
Sokoine-Kibaoni, Morogoro: Wananchi eneo la Sokoine-Kibaoni, Wilaya ya Mvomero, Morogoro mpaka sasa bado hawajaanza kupiga kura mbali na wengi wao kujitokeza huku wengine wakiwa wamekodi magari kutoka Bwawa la Kihonda umbali wa kilomita 20 kwenda kupiga kura lakini mpaka sasa bado hawajapiga kura.
Amana, Ilala: Baadhi ya wananchi wameamua kususia zoezi la upigaji kura katika Kituo cha Amana, Ilala jijini Dar baada ya mgombea Uenyekiti wa Mtaa wa Amama aitwaye Mathias Ijumba kuondolewa katika uchaguzi dakika za mwisho kwa kile kinachodaiwa kuwa si mkazi wa eneo hilo lakini jambo la ajabu jina like liko katika orodha ya watu waliojiandikisha kupiga kura na mgombea huyo ameruhusiwa kupiga kura yake.
Baadhi ya wananchi wa eneo hilo wamedai jamaa huyo anakubalika sana na huenda ndiyo chanzo cha jina lake kuondolewa.
Dar es Salaam: Wananchi katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam wanalalamikia utaratibu wa majina unaotumika katika zoezi la upigaji kura linaloendelea, wengi wadai kupata tabu kuona majina yao huku wengine majina yao yakiwa hayapo kabisa katika vituo.
Shariff Shamba, Ilala: Eneo la Shariff Shamba, Ilala jijini Dar uchaguzi umeahirishwa mpaka Jumapili ijayo baada ya vifaa kutopatikana ndani ya muda muafaka. Vyama vyote vinavyoshiriki vimeafikiana.
Kagunga, Kigoma Kaskazini: Uchaguzi katika Vijiji vya Zashe na Kagunga, Kata ya Kagunga, Jimbo la Kigoma Kaskazini umefutwa hadi itakapotajwa tena baada ya Mtendaji wa Kata kuwaengua ACT katika uchaguzi huo baada ya kudaiwa kuwa wagombea wawili wa vijiji hivyo kutoka ACT walitumia anuani ya shule kama anuani yao. Hata hivyo Msimamizi Mkuu amesema anafuta uchaguzi hadi watakapotangaza tena.

CHANZO: GPL

No comments

Powered by Blogger.