MKURUGENZI MAHAKAMANI KWA KUVURUGA UCHAGUZI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimemfikisha mahakamani Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, Lucas Mweri, kwa madai ya kuvuruga uchaguzi wa serikali za mitaa na kusababisha zaidi ya vijiji 80 kutofanya uchaguzi huo uliyofanyika Desemba 14, mwaka jana.
Mweri ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi huo amefikishwa kizimbani pamoja na wasimamizi wasaidizi wa vijiji na Kata za Wilaya hiyo.
Katika madai yaliyowasilishwa na mwanasheria wa Chadema, Frederick Kihwelo, mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Korogwe, A.J Kirekiano ni kwamba wasimamizi hao walivuruga kwa makusudi uchaguzi huo na kusababisha zaidi ya vijiji 80 kutofanya uchaguzi huo.
Chama hicho kinaeleza kuhujumiwa katika uchaguzi huo kwa wagombea wakekuenguliwa dakika za mwisho bila kufuatwa kwa kanuni, taratibu na sheria ya uchaguzi.
Hata hivyo kesi hiyo imeairishwa baada ya kutajwa na kupangiwa kusikilizwa Februari 18, mwaka huu.
Wakielezea sakata hilo baada ya kesi hiyo kuairishwa, Katibu wa Chadema, jimbo la Korogwe Vijijini, Salum Sempoli, alisema vijiji 98 vya jimbo hilo havikufanya uchaguzi baada ya wagombea wao kuenguliwa na msimamizi wa uchaguzi.
Sempoli alieleza kuwa mkurugenzi huyo wa halmashauri akiwa msimamizi wa uchaguzi aliwaengua visivyo halali wagombea wa nafasi za uenyekiti wa vitongoji na vijiji sambamba na wajumbe bila sababu za msingi.
CHANZO: NIPASHE

No comments

Powered by Blogger.