MWENYEKI WA SHIRIKISHO LA WAFANYABIASHARA APANDISHWA MAHAKAMANI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


  Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya Wafanyabiashara Nchini, Bw. Jonson Minja aliyevaa koti akisindikizwa katika mahakama ya mkoa wa Dodoma chini ya ulinzi wa askari polisi.
Mweyekiti wa Shirikisho la vyama vya Wafanyabiashara Nchini, Bw.  Jonsoni Minja aliyevaa koti huku akiongea na katibu wake Mchungaji Kiondo akisubili kusomewa mashitaka yake mawili likiwemo la kuchochea Wafanyabiashara  wasilipe kodi ya Serikali  katika mahakama ya mkoa wa Dodoma.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya Wafanyabiashara Nchini, Bw.  Jonsoni Minja akisomewa mashataka yake katika mahakama ya mkoa wa Dodoma.


Na John Banda,Dodoma
MWENYEKITI wa Shirikisho la vyama vya Wafanyabiashara Nchini Jonson Minja  amefikishwa Mahakama ya Mkoa wa Dodoma kwa Mashitaka mawili ikiwemo la kuchochea Wafanyabiashara  wasilipe kodi ya Serikali.
Akisoma Mashitaka hayo Wakili wa Serikali Gogfrey Wambari mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Rebbeka Mbiru alisema mtuhumiwa alitenda makosa hayo tarehe 6 Septemba 2014 alipokuwa katika mkutano na Wafanyabiashara katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma.
Wambari alisema Mtuhumiwa alitenda makosa mawili ya Kushawishi Wafanyabiasha kutenda kosa la jinai na kosa la pili kuzuia ukusanyaji wa Kodi kwa kutumia Mashine za Kielotroniki EFD.
‘’Kifungu cha 390 kinasomeka pamoja na kifungu cha 35 cha Sheria ya adhabu sura ya 16 ni  kosa kushawishi vitendo vyovyote vya jinai’’
‘’Kifungu cha 107 kifungu kidogo C cha Sheria ya kodi sura ya 332 ya mwaka 2004 ni kosa kuzuia ulipaji wa Kodi ya Serikali ‘’alisema Wambari.
Aidha Wambari alimtaka Hakimu kuzingatia umbali wa anakoishi mtuhumiwa wakati atakapokuwa akitoa masharti ya dhamana. Kwa upande wake Mtuhumiwa wa Kesi hiyo Jonson Minja 34 alipoulizwa makosa hayo na Hakimu alikana mashitaka yote. Hata hivyo hakimu wa Mahakama hiyo Rebbeca Mbiru alitoa masharti ya
dhamana ya Mtuhumiwa kwa kusema kuwa anatakiwa awe na Wadhamini wawili mmoja wapo akiwa mtumishi wa Serikali na wote wawili wawe na vitu wenye   dhamani isiyopungua Milioni nne.
‘’Dhamana ipo wazi kwa mtuhumiwa kinachotakiwa awe na wadhamini wawili wenye mali zisizohamishika zenye dhamani isiyopungua milioni nne’’
Kwa upande wake Wakili  anaemtetea Mtuhumiwa Godfrey Wasonga, alimtaka Hakimu kuzingatia haki ya Mtuhumiwa kutokana na kuwa ni mtu anaeaminiwa na Wafanyabiashara kote Nchini hivyo hataweza kutoroka masharti ya dhamana yasiwe magumu. Hata hivyo hakimu Rebbeka Mbiru ameahirisha kesi hiyo hadi tarehe 11 mwezi wa pili 2015 shauri hilo litakapo somwa tena.

No comments

Powered by Blogger.