MPYAAAA: ANGALIA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE HAPA YA 2014

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini,Dk. Charles Msonde akizungumza na wanahabari jijini dar leo.

Na Chalila Kibuda
Shule za sekondari za binafsi zaongoza 10 bora matokeo ya mtihani wa  kidato cha nne uliofanyika mwaka jana.
Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini  (NECTA), Dk.Charles Msonde amesema katika matokeo ya kidato cha nne ya mtihani wa mwaka jana ufaulu umeongezeka  kwa asilimia 12.67 ikilinganishwa na mwaka 2013.
Katika matokeo hayo msichana wa shule ya sekondari ya Baobab, Nyakaho I. Marungu ndio aliyeongoza mtihani huo na kufatia wavulana.
Shule za Sekondari za St.Fransis ya mkoani Mbeya wanafunzi sita na Feza wanafunzi nane na kufanya shule hizo kuingia katika 10 bora kwa kutoa idadi wanafunzi wengi ikilinganishwa na shule zingine.
Msonde amasema matokeo hayo  yanatokana na mfumo mpya  wa GPA kwa kuangalia masomo saba  hivyo ufaulu umetokana na mfumo huo.








No comments

Powered by Blogger.