WAFANYAKAZI WA MFUKO WA LAPF WAFANYA BONANZA LA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA WA 2015 MJINI DODOMA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Wafanyakazi wa mfuko wa Pensheni wa Serikali za mitaa (LAPF) wakishangilia wakati walipokuwa wakiingia kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari ya Dodoma walipokutana kwa ajili ya michezo ya Bonanza la kuukaribisha mwaka Mpya.
 Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni ya Serikali za Mitaa (LAPF) wakishindana kufukuza kuku wakati wa Bonanza la wafanyakazi hao waliotoka kwenye kanda tofauti hapa nchini ambazo ni  kanda ya Ziwa, kanda ya kaskazini na kanda ya kati walipokuwa wakiukaribisha mwaka mpya.

 Wafanyakazi wa LAPF wakimenyana katika mchezo wa mpira wa pete walipokuwa kwenye Bonanza kabla ya kukutana kwanye hafra ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2015 kwenye viwanja vya shule ya Sekondari ya Dodoma.
 Wafanyakazi wa LAPF kanda ya Ziwa na Makao makuu wakioneshana umahiri wao kwenye mchezo wa mpira wa miguu walipokuwa  kwenye Bonanza la kuukaribisha mwaka mpya wa 2015 ambapo Wafanyakazi wa Makao Makuu walishinda bao 5 - 1 mchezo uliopigwa kwenye  uwanja wa Shule ya Dodoma Sekondari.
Baadhi ya Wafanyakazi wa mfuko wa Pensheni wa Serikali za mitaa (LAPF) wakivuta kamba kwenye mashindano ya uvutaji wa kamba kwenye Bonanza lao lililofanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari ya Dodoma (PICHA NA JOHN BANDA)

No comments

Powered by Blogger.