ASKOFU GWAJIMA AACHIWA KWA DHAMANA, ANENA YA MOYONI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.



Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akiwa kwenye baiskeli ya wagonjwa Hospitali ya TMJ Dar es Salam leo mchana akielekea  Kituo cha Polisi cha Oyterbay kupewa dhamana.
Hapa Askofu Gwajima akiingia kwenye gari huku akiwa na maumivu makali wakati akielekea kwenye kituo hicho kupewa dhamana 

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Wachungaji wakibadilishana mawazo wakati wakimsubiri Askofu Gwajima apewe dhamana
Waumini wa kanisa hilo wakijiandaa kumpokea Askofu wao baada ya kupatiwa dhamana
waumini hao wakiwa kituoni hapo.
Waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima wakiwa wamelizonga gari lililombeba Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Josephat Gwajima, huku wakishangilia kwa kusema yesu yesu baada ya kupewa dhamana  katika Kituo cha Polisi Oysterbay Dar es Salaam leo mchana.
Waumini hao wakilipungia mkono gari lililomchukua  Askofu Gwajima.
Wanahabari wakitoka kituo cha polisi Oysterbay kufuatilia habari hiyo. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

        Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima (pichani) ni sawa na sikio la kufa ambalo alisikii dawa, baada ya leo kuibuka na kusema haogopi kulitetea tamko lililotolewa na jukwaa la kikristo nchini ambalo linawahamasisha waumini wa dini hiyo kuipigia kura ya hapana katiba iliyopendekezwa na Bunge  Maalum la katiba, ambapo amesema atalipinga hata kama serikali ikimwekea vikwazo vya aina yoyote.
           Kauli kiongozi wa huyo wa Kiroho ameitoa muda huu kwenye Makao Makuu ya Jeshi la polisi mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni ambapo alipojisalimisha ili kuhojiwa kwa mara ya mwisho baada ya kutoka kwenye Hospitali ya TMJ, Mikocheni jijini Dar es Salaam alipolazwa kutokana na kuugua gafla wakati akiwa kwenye mahojiano na Jeshi la polisi wiki iliyopita.

      Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuhojiwa na Jeshi la Polisi wilaya ya Kinondoni na ameachiwa kwa dhamana na jeshi hilo huku akitakiwa kufika katika kituo kikuu cha polisi april 02, 2015 kwa ajili ya kuendelea na mahojiano na jeshi la polisi huku waumani wake kijitokeza na kumpokea Askofu wao. Ambapo amesema hawezi kutishika wala kuyumbika kutokana na vikwazo anavyowekewa na Serikali juu ya kuwatetea wakristo  hapa nchini ambao wamewekewa Katiba anayoiita ni mbovu.

         “Mimi nimetoka kwa amani nashukuru sana mungu animeponya salama, ila nasema sitoacha kusema ukweli juu ya wakristo wenzangu ambao wanakandamizwa na mifumo ya Katiba ambayo inaonekana wazi”Amesema Askofu Gwajima.
          Askofu Gwajima ameongeza kuwa kwa kuwataka viongozi wenzake kuheshimu tamko la Jukwaa la Kikristo na hata  yeye mwenyewe amesema ataliheshimu sana.

        “Nawaamomba viongozi wa dini wenzangu tuliheshimu tamko hili la kikristo, na endapo tukiwa tofauti tutakuwa tunakwenda tofauti na tunajivunjia heshima kwa jamii ambapo tulionekana kuwa na msimamo mmoja wakati tukilitoa na mimi mwenyewe nawahakikishia nitalitetea mpaka mwisho” ameongeza Gwajima.
           Alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu afya yake amesema hawezi kuzungumzia afya yake, akawataka waandishi kutoendelea kumuuliza huku akiwataka waumini wake kushangilia kwa ushindi waliupata anadai umetokana na nguvu ya mungu.
Kabla ya kulazwa katika Hospitali ya TMJ, Askofu Gwajima alipelekwa katika Hospitali ya Polisi Kurasini na baadaye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambapo yeye na wafuasi wake waligoma na kutaka atibiwe TMJ ambapo kuna daktari wake maalumu.

STORI NA NA KAROLI VINSENT


No comments

Powered by Blogger.