MWILI WA ABDUL BONGE WAPELEKWA MUHIMBILI KWA UCHUNGUZI ZAIDI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Mwili wa aliyekuwa mwanzilishi wa Kundi la Tip Top Connection, Abdu Bonge, leo asubuhi ulihamishwa kutoka katika Hospitali ya Mwananyamala na kupelekwa Muhimbili kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi.
Mtandao huu ulishuhudia jamaa wa marehemu huyo wakiuhamisha mwili huo wakisema ni lazima mwili huo ukafanyiwe uchunguzi wa kina kutokana na utata wa kifo chake. Mdogo wa marehemu aitwae Idd Taletale alisema endapo uchunguzi huo utamalizika leo utasafirishwa leo kuelekea Kijiji cha Mkuyuni kilichopo Matombo mkoani Morogoro kwa ajili ya mazishi.
CHANZO: GPL

No comments

Powered by Blogger.